Na Scolastica Msewa, Kibaha
Shule ya uongozi ya Mwalimu Julias Kambarage Nyerere ya Kibaha mkoani Pwani imekutanisha wawakirishi wa Chama Cha kikomunisty cha nchini China CPC na Wataalamu wabobezi toka vyuo vikuu kadhaa nchini kujadili maboresho ya mahusiano ya kimaendeleo Kati ya Tanzania na China ili tunufaike kiuchumi hata kupiga hatua za Maendeleo kama taifa Hilo.
Semina hiyo ya siku moja imefanyika Shule ya uongozi ya Mwalimu Julias Kambarage Nyerere huko Kibaha mkoani Pwani ambapo Wataalamu hao wabobezi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini wamekutana kujadili ya kufanyia maboresho katika sekta ya kilimo, uvuvi, utalii na ujenzi ili Tanzania na Afrika kwa ujumla tuendelee kunufaika na uhusiano wa nchi ya China na Chama Cha CPC.
Mkuu wa Shule ya uongozi ya Mwalimu Julias Kambarage Nyerere Prof. Macelina Chijoriga amesema yapo mambo kadhaa mazuri ya kujifunza sisi taifa la Tanzania yakiwemo masuala ya ya uchumi na ya kijamii toka nchini China ilikujua namna China walivyofanikiwa tangu walipotokea kimaendeleo kuanzia miaka ya sitini hadi kufikia hatua iliyopo hivi sasa ambapo tulifanana kiuchumi.
Mwakirishi wa Chama Cha kikomunisty cha nchini China CPC Komredi Jin Xin amesema China wamekuwa na ushirikiano na nchi za Africa kwa kuimarisha mawasiliano na mahusiano na kwamba wanamengi ya kushirikiana na Tanzania na Bara Zima la Afrika katika sekta ya kilimo, uvuvi, utalii na miundombinu.
Amesema kujengwa kwa Shule hiyo ya uongozi ya Mwalimu Julias Kambarage Nyerere kwaajili ya Vyama sita vya harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Africa ni Moja ya mfano mzuri wa Tanzania na nchi ya China.
Mmoja wa wabobezi hao waliokuwa katika majadiliano baina yao na wataalamu tokw China kanali mstaafu George Simbakaria amesema jambo mojawapo la kujifunza ni namna walivyotengeneza vizazi vyenye uadilifu na uwaadilifu kuanzia utotoni.
Amesema ili kutoa viongozi bora ni lazima malezi ya watoto na vijana kwakulelewa toka chini kuwa waadilifu na waaminifu kwa taifa lao na sio kuendeleza vitendo vya kutokuwa na uwaadilifu na uaminifu kwa taifa letu.
Kanali Mstaafu Simbakaria amesema jambo kubwa la kujifunza kwa China ni kwamba mafanikio yake hayakutokana na ukoroni kama ilivyokuwa katika mataifa mengine makubwa ambayo yaliwahi kutawala katika koloni mbalimbali barani Africa na mataifa mengine duniani.
Mkuu wa Kituo cha tafiti za uchumi na jamii nchini Dkt. Hoseana Lunogelo amesema nchi ya China shughuli zake za kimaendeleo na shughuli za chaguzi hazina kabisa tuhuma za rushwa hivyo tunaweza kujifunza kwao namna ya kuboresha na kudhibiti vitendo vya rushwa katika taifa letu na Bara Zima la Afrika.
Ameshukuru kwa uongozi wa China kwa kutoa fursa ya kutoa elimu ya kudhibiti mianya ya rushwa katika sekta zote kwa Tanzania na Bara Zima la Afrika.
Naye Mhadhiri toka Chuo cha Mwalimu Julias Kambarage Nyerere Nyerere kampasi ya Zanzibar Dkt Rose Mbwete amongeza kuwa Watanzania tuna vingi vya kujifunza kutoka taifa la China ili watanzania kufikia hatua ya maendeleo kama nchi ya China iliyo nafasi ya pili duniani ni kufanya kazi kwa bidii na kuwa na miongozo dhabiti inayodhibiti vitendo vya rushwa.
Awali Prof. Chijoriga amesema Tanzania na nchi ya China tuna mahusiano ya Moja kwa Moja kupitia CCM na Tanzania kwa ujumla na mahusiano Bora baina ya Nchi zote sita za harakati za Ukombozi wa nchi za kusini mwa Africa ambapo ni Angola, Namibia, Msumbiji, Africa kusini, Zimbabwe ambapo alishukuru kwa mahusiano hayo mazuri ambayo yaliwezesha kujengwa kwa Shule hiyo ya uongozi ya Mwalimu Julias Kambarage Nyerere hapo Kibaha mkoani Pwani.
Amesema semina hiyo ya kwanza ni kwa lengo la majadiliano ni maandalizi ya mkutano mkubwa utaotarajia kufanyika hapo baadaye mwaka huu baina ya nchi hizo mbili marafiki ambao pia kupitia semina hiyo wangependa kujua nini wanaweza saidia Tanzania na Bara Zima la Afrika.
0 Comments