Na Ibrahim Yassin Matukio App -Songwe
Mbunge wa Jimbo la Momba, Condester Sichalwe (Mundy) aongoza timu ya wataalamu akiwemo Afisa Madini mkazi Mkoa wa Songwe Chone Malembo kwenda kushuhudia utafiti wa madini ya Sodalite yaliyobainika eneo jimboni kwake Kijiji Cha Chindi.
Mbunge Condester amempongeza mchimbaji mdogo wa madini ya Sodalite Nicko Laus Buseni kwa kuamua kufanya utafiti wa madini hayo ndani ya Jimbo lake na kueleza kuwa yupo tayari kumuunga mkono, ikiwa ni pamoja na kumkutanisha na taasisi za kifedha ili apatiwe Mkopo.
Condester amewasihi wananchi wa kijiji cha Ntinga na Momba kwa ujumla kuchangamkia fursa ya kupata leseni kwa ajili ya uwekezaji wa madini ya Sodalite amb ayo yanadaiwa kugundulika kijiji cha Chindi Kata ya Msangano.
Afisa Madini Mkazi mkoa wa Songwe, Chone Male mbo, amesema madini ya Sodalite yanafanyiwa utafiti kijiji cha Chindi Kata ya Msa ngano Wilaya ya Momba, yatakuwa ni madini mapya kupatikana ndani ya Mkoa huo, kwani hakuna eneo jingine yanayopatikana madini hayo ndani ya Momba.
Mkoa wa Songwe ni miongoni mwa mikoa yenye fursa za madini yakiwemo madini adimu hivyo ipo haja vijana kuchangamkia fursa za uchimbaji kuongeza kipato.
0 Comments