Shirika la sauti ya haki Tanzania la mfungulia akaunti ya benki mjane Maria Ngoda ili kuwezesha wadau mbalimbali wa maendeleo kuchangia fedha kwaajili ya biashara na matumizi binafsi.
Matukio Daima media mahojiano na wakili Leticia Petro Ntagazwa ambaye ni mkurugezi wa shirika la sauti ya haki Tanzania ameitaja akaunti hiyo, 0152869072900 kupitia benki ya CRDB na kusema lengo la akaunti hiyo ni kuweka uwazi kwa wachangiaji ambao watakuwa wanatuma fedha kwaajili ya kumsadia Maria, hivyo amewaomba wadau na watanzania kwa ujumla walioguswa na hali ya Maisha ya mjane huyo kuchangia kiasi chochote cha fedha kupitia akaunti hiyo.
Wakili Ntagazwa ameelezea malengo ya shirika hilo katika kumpatia elimu itakayo msaidia kuweza kusimamia biashara ambayo ataifungua kupitia fedha ambazo atazipata kutokana na mtazamo alikuwa nao hapo awali mwana mama huyo wakufanya biashara ndogo ya kuuza Samaki.
“Pindi fedha hizo zitakapo patikana shirika la sauti ya haki Tanzania tumepanga kumpatia elimu ya biashara Maria kwani ananokana hana uelewa juu ya biashara kubwa kwani hata mwanzo tulipo muuliza alisema anahitaji mtaji wa shilingi laki moja na nusu ili aweze kufanyabiashara ya Samaki”.
Akizungumzia kiwango wanachokitarajia kupata ili kuweza kufanikisha malengo ya kufungua biashara na kwa ajili ya matumizi binafsi amesema kiwango cha chini ni shilingi milioni tano.
Katika hatua nyingine ameongelea swala la kumsaidia Maria Ngoda kiuchumi, na kusema kuwa shirika la sauti ya haki Tanzania limekuwa likiwasaidia wanawake wengi wenye hali ngumu za kiuchumi, ili kuweza kuhudumia familia zao.
“siyo Maria peke yake shirika letu limekuwa likisaidia wanawake mbalimbali wanao pitia changamoto mbalimbali za kiuchumi kama mwezi ujao tuna wanawake 10 ambao watapatiwa mitaji kwaajili ya kuanzisha biashara, lakini Maria amekuwa na bahati sana kuanzia siku ya hukumu yake mpaka sasa”.
0 Comments