Header Ads Widget

TRENI YA UMEME YAANZA MAJARIBIO DAR - MORO

Na fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar

Shirika la Reli Tanzania (TRC) leo limeanza safari ya kwanza ya majaribio kwa Treni ya umeme ya Abiria (SGR)  kutoka ofisi zake zilizopo jengo la Tanzanite maeneo ya stesheni Jijini Dar es salaam kuelekea Mkoani Morogoro.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini humo mapema leo hii Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Masanja kadogosa amesema Usafiri huo wa Treni utatumia umeme wa kawaida kutoka TANESCO na wanatarajia kuanza safari za abiria hivi karibuni.

Aidha amewatoa wasiwasi watanzania wanaodhania kuwa umeme ukikatika utaweza kuleta athari kwa Treni hizo kuwa sio kweli umeme wake umeunganishwa kutoka grid ya taifa hivyo si rahisi umeme kukatika kwenye njia ya Treni.


Ameongeza kuwa,katika majaribio hayo walimeambatana pamoja na msemaji wa Serikali, wasanii, waandishi wa habari, wahariri na baadhi ya wafanyakazi wa TRC, ambapo treni hiyo ina uwezo wa kutembea Km/h100-160.

Kwa upande wake, Msemaji Mkuu wa Serikali Mohbare Matinyi amesema kuwa, ujio wa treni hiyo ya mwendokasi utakua fursa kwa wananchi wa morogoro na Dar es Salaam ambapo zoezi hilo litafanyika kwa mikoa yote ambayo itapitiwa na mradi huo.


"Leo tumeweza kuanza hatua ya majaribio kwa treni yetu ya abiria kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro, miezi michache ijayo treni hii itaanza safari zake hadi kufika Dodoma ni jambo la kupongeza kwa Serikali yetu, hii inatoa fursa za kiuchumi wananchi wetu wanatakiwa wafanye biashara na mradi huu utakapokamilika tutaweza kufanya biashara na nchi jirani"

Ameongeza kuwa "Treni ni usafiri wa usalama na uhakika na wa bei nafuu, hapa biashara zitafanyika wananchi watafaidika kwa kazi nzuri iliyofanywa na Serikali kwa mfano Mkoa wa Dar es Salaam sio wakulima kwa hiyo watachukua mazao kutoka Morogoro, Morogoro wataletewa bidhaa za kiwandani kutoka Dar es Salaam ambapo zoezi hilo litafanyika pia na kwa mikoa mengine mradi ukikamilika"amesema Matinyi.


Imeondoka majira ya saa 10:30 asubuhi katika ofisi zake za Tanzanite (Stesheni) jijini Dar es Salaam na kufika Morogoro majira ya 12:47 mchana ambapo imefanya tena safari ya kurudi Dar es Salaam kutoka Morogoro 1:47 .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI