Wafuasi wa Chama Cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA )Kanda ya Nyasa wametoa Salam za pole kufuatia kifo Cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Ngoyai Lowasa kilichotokea mapema hii Leo .
Akitoa Salam za pole Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msingwa amesema ni mstuko na pigo kwa Taifa , watamkumbuka kwa mema mengi ikiwemo kupigania uanzishwaji wa shule za Sekondari Kila Kata, kiongozi mahiri , mwenye maono na kusimamia ndoto zake.
Msigwa ni miongoni mwa watu aliofanya nao kazi za kisiasa mwaka 2015 alipowania nafasi ya U-Rais kwa tiketi ya Chama Cha demokrasia na Maendeleo Chadema,huku yeye akiwa mratibu wa mikutano ya kampeni.
0 Comments