Mahakama ya Paris nchini Ufaransa imemhukumu aliyekuwa kiongozi wa waasi wa Congo, Roger Lumbala, kifungo cha miaka 30 jela kwa kuhusika na uhalifu uliotekelezwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya mwaka 2002 na 2003.
Lumbala alikuwa kiongozi wa kundi la waasi la RCD-N, ambalo lilitekeleza operesheni ya kikatili iliyopewa jina la "Futa Kila Kitu.
Mahakama hiyo ilimpata Lumbala na hatia ya kushiriki katika uhalifu dhidi ya binadamu, ama kwa kutoa amri moja kwa moja au kwa kusaidia na kuhamasisha wanajeshi wake kutekeleza vitendo hivyo.
Waendesha mashtaka wameomba ahukumiwe kifungo cha maisha, lakini majaji waliamua kumpa adhabu ya miaka 30 jela.






0 Comments