NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, Prof. Patrick Ndakidemi ameonyesha nia ya dhati ya kuwapigania wananchi wa Jimbo hilo na kuwaletea maendeleo.
Hili limejidhihirisha wazi kwa Mbunge huyo kupambana Bungeni na kuishawishi serikali kupeleka miradi mbambali katika jimbo hilo.
Sekta mbalimbali amekuwa akipambana nazo ikiwemo Afya, Barabara, Elimu, Maji, Utawala.
Katika kudhihirisha hilo katika miaka mitatu ya uongozi wa Mbunge huyo amefanikiwa kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya Tarafa ya Hai mashariki katika kata ya Kimochi.
Wananchi wa Tarafa ya Hai mashariki wamemshuku Mbunge pamoja na Madiwani kwa kuwapigania miradi huo ni kielelezo.
Mwisho.
0 Comments