Header Ads Widget

TULEE VIJANA KATIKA MISINGI YA HAKI, UPENDO NA KUPENDA KAZI- DC MTAMBULE


Jamii, walezi na wazazi nchini Tanzania wametakiwa kuhakikisha wanawalea watoto katika misingi ya upendo, amani, kufanya kazi na kuhakikisha wanakuwa na mchango katika Taifa kama sehemu ya kuimarisha amani na mshikamano wa Jamii na Taifa kwa ujumla.

Wito umetolewa leo Jumamosi Disemba 27, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar Es Salaam Mhe. Saada Ahmed Mtambule wakati wa kongamano la kidini lililofanyika Mkoani Dar Es Salaam, likijadili kuhusu amani, ustawi na maendeleo ya Jamii na Tanzania kwa ujumla wake.

"Tujiulize ni mara ngapi katika wiki, mara ngapi katika mwezi sisi waumini tumekaa Baba, Mama na Watoto tunasoma Vitabu vyetu vya dini, tukatafakari mafundisho ya Mtume wetu, mara ngapi tumekaa na Vijana na watoto wetu tukazungumza masuala yanayowahusu wao na Taifa kwa ujumla na familia juu ya kuimarisha upendo, amani, kufanya kazi na kuwa na mchango kwenye Taifa letu? Tukiweza kufanya haya amani na upendo utakuwepo na matukio mengine ya rushwa na uhalifu utaweza kupungua." Amesema Mhe. Mtambule.

Mhe. Mtambule kadhalika katika hotuba yake amesisitiza umuhimu wa familia kukaa, kujadili, kusoma na kutafakari maandiko matakatifu huku pia wakijadili kuhusu namna ya kuimarisha Amani, Upendo na kuwa na mchango katika Taifa ili kuondoa changamoto za kijamii na kisiasa ambazo zimekuwa zikitokea katika maeneo mbalimbali nchini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI