Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imemuacha huru Mke wa Marehemu Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na Mfanyabiashara Revocatus Everist baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yao.
Wawili hao walifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza February 23 ya mwaka 2017 wakikabiliwa na kesi ya jinai namba 103 wakituhumiwa kumuua mdogo wa Bilionea Msuya, Aneth Msuya kwa kumchinja Kigamboni, May 26, 2016.
"Baada ya kujiridhisha pasina kuacha shaka, Mahakaa hii inawaachia huru wawili hawa kutokana na upande wa mashtaka kutothibitisha makosa dhidi yao,"
"Kuhusu gari Land Rover lililotolewa Mahakamani kama kielelezo sio sehemu ya familia hiyo, gari litataifishwa na Serikali”
0 Comments