MGOMBEA wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Juma Duni Haji ametaja sababu zilizomsukuma kujitosa kuwania Nafasi hiyo ya uongozi katika Chama hicho ikiwa ni pamoja na kujenga na kuendeleza Umoja kitaifa.
Aidha ameeleza kuwa, dhamira yake kuendeleza chama hicho na kufikia malengo waliojiwekea ya kushika dola.
Akihutubia mamia ya Wanachama na Wafuasi wa Chama cha ACT Wazalendo leo Vuga mara baada ya kurejesha fomu amesema kuwa nia yake kuunganisha chama, kuendeleza Umoja wa kitaifa uliopo hivi sasa.
"Nimefanya kazi kubwa katika Chama hichi hivyo nmegombea ili kuendeleza pale nilipoishia kuhakikisha tunawahamasisha wakina mama na Vijana wengi zaidi kujiunga na Chama cha ACT -Wazalendo," amesema Babu Duni.
"Chama hichi kwa sasa kimekuwa Chama kikubwa kutokana na Kazi tulioifanya Mimi na wenzangu nimegombea ili kuendeleza pale tulipoishia ya kujenga Chama Chetu," amefahamisha.
Hata hivyo Juma Duni Haji ambae pia Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa ameiomba viongozi wa Chama hicho kuhakikisha Uchaguzi unakuwa wa haki ili kuendeleza Umoja ndani ya Chama hicho.
Mapema Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Mjini Kichama Haji Dude ameiomba Wachama wa Chama hicho kuwa wamoja na kutogawanyika.
0 Comments