Header Ads Widget

WAJANJA WAJANJA WA DAWA ZA BINADAMU NA MIFUGO NJOMBE KUDHIBITIWA

Anitha Mshighati  Meneja wa TMDA kanda ya nyanda za kusini
Mwakilishi wa katibu tawala mkoa wa Njombe Lewis Mnyambwa
Washiriki wa mafunzo ya TMDA  mkoa wa Njombe

xxxxxxxxx

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Serikali mkoani Njombe imewaonya wafanyabiashara wa dawa za binadamu na mifugo wanaotaka kupata kipato kikubwa katika uuzaji wa bidhaa hizo kwa kukiuka sheria za nchi kwa kumkandamiza mlaji wa mwisho.


Katika mafunzo kwa wamiliki wa maduka ya dawa za binadamu na mifugo pamoja na wafamasia chini ya Mamlaka ya dawa na vifaa tiba Tanzania TMDA Mwakilishi wa Katibu tawala mkoa wa Njombe Lewis Mnyambwa wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo amesema hatua za kisheria zitaendelea kuchukuliwa kwa yeyote atakaye kiuka sheria kwa lengo la kutaka kujipatia kipato zaidi.

Meneja wa Mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA Kanda ya nyanda za juu kusini Anitha Mshighati anasema kutokana na kuwapo kwa baadhi ya wafanyabiashara wadanganyifu ambao wamekuwa wakisababisha madhara kwa jamii wamelazimika kuchukua hatua ya kutoa elimu katika mikoa yote ya kusini ili kukabiliana na changamoto hiyo.


Baadhi ya wamiliki wa maduka ya Dawa za binadamu na mifugo mkoani Njombe akiwemo Kenedy Msemwa,Helimerinda Saganda,Daines Sambo na Ester Igembe wamekana kuuza dawa zisizo sajiliwa na zilizochini ya kiwango[Feki ]huku wakitaka TMDA kuongeza nguvu ya udhibiti   kwani baadhi yao wanajiingiza kwenye biashara hiyo kwa lengo la kujipatia kipato kwa njia za mkato. 


Hata hivyo TMDA imesema tayari imeshawachukulia hatua wafanyabiashara mbalimbali kwa kuteketeza bidhaa feki,kuwatoza faini kwa mujibu wa sheria kusini mwa Tanzania hususani kwa wale waliobainika kukiuka sheria za Mamlaka hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI