Na Thobias Mwanakatwe, MKALAMA
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida limepitisha kwa kauli moja makisio ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 jumla ya Sh.bilioni 29.966 ambazo zitatumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ruzuku ya mishahara na matumizi mengineyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Messos, akiwasilisha baheti hiyo kwenye kikao hicho, alisema maeneo yaliyopewa kipaumbele ni kuongezeka kwa mapato ya ndani kutoka Sh.bilioni 1.739 mwaka 2023/2024 hadi kufikia Sh.bilioni 2.430 mwaka 2024/2025 ambalo ni ongezeko la Sh.milioni 691.388 sawa na asilimia 39.7.
Alisema katika bajeti hiyo Sh.bilioni 3.576 zitatumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo vipaumbele ni kukamilisha miradi inayoendelea kutekelezwa ili iweze kutoa huduma kabla ya kuanza miradi mipya,ulipaji wa madai ya malimbikizo ya mishahara kwa watumishi wa umma.
Messos alisema vipaumbele vingine ni kutenga bajeti kwa ajili ya elimu ya kutoa elimu ya uhamasishaji kwa wakulima,wafugaji na wavuvi kwa kushiriki katika ujenzi wa miundombinu hiyo na stability za watumishi ambazo ni mishahara,malimbikizo na uhamisho.
Mkurugenzi huyo alisema shughuli muhimu zitakazotekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani ni ukamilishaji wa vyumba vitatu vya madarasa kwa shule za msingi za Endasiku,Kinankamba na Mdilika,kujenga matundu matano ya vyoo katika shule ya sekondari ya Gracemesaki.
Shughuli nyingine ni kununua vitanda kwa ajili ya hosteli ya Shule ya Sekondari Jorma,kusaidia ukamilishaji wa ofisi mbili za kata,kukamilisha zahanati za Ibaga na Kenke,ujenzi vyoo katika minada ya Kikhonda,Hilamoto na Mkalama,ujenzi wa uzio katika minada hiyo,kuboresha stendi y Iguguno na Nduguti na kuendelea kutenga na kutia mikopo kwa wanawake,vijana na walemavu.
Alisema katika bajeti iliyopita ya 2023/2024 katika kipindi cha Julai hadi Disemba mafanikio yaliyopatikana ni kutekelezwa mirafi yenye thamani ya Sh.bilioni 1.198 katika sekta ya elimu,kusajili shule mpya za sekondari,kuajiri watumishi wapya kwa ajira ya kudumu 56,kuthibitisha kazini watumishi 44,kupandisha vyeo watumishi wapya 103 na kuwaendeleza watumishi 27 za kimasomo.
Aidha, Mkurugenzi huyo aliwaomba madiwani wasaidie katika usimamizi wa miradi inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ili miradi hiyo iweze kuwa na tija kwa wananchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea 2024/2025.
"Ni ngumu kwa Mhandisi kufika kila eneo kwasababu hivi sasa tuna miradi kila kata na kila kijiji hivyo madiwani wakitusaidia katika usimamizi itaweza kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi," alisema.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama,James Mkwega, akifunga kikao hicho aliwaomba madiwani kusaidia kutoa ushirikiano ukusanyaji wa mapato badala ya kuwaachia watendaji pekee yao.
Mkwega aliwataka pia watendaji kupeleka maandiko ya bajeti katika miradi mingi bila kuona aibu ili kama ni kuenda kuchujwa ikafanyike huko.
Katika hatua nyingine madiwani wilayani Mkalama mkoani Singida wameiagiza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) kuanzisha operesheni ya kukamata mifugo inayopitishwa kwenye barabara na kuwatoza faini wahusika ili kulinda na kuheshimu miundombinu hiyo isiendelee kuharibiwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega alisema zipo sheria ndogo za halmashauri ambazo zinaweza kutumika kuwatoza faini wanaopitisha mifugo barabara na kufanya uharibufu wa miundombinu hiyo.
"TARURA wekeni kila mtu kila kata na ikiwezekana muwape na pikipiki ambao watakuwa wanafanya patro kwenye barabara zetu au hata mkitafuta watu binafsi wakafanya kazi hiyo mnakubaliana katika faini atakayotozwa mwenye mifugo anapewa kiasi fulani mkamataji hii itakomesha tatizo hili," alisema.
Naye Diwani wa Kata ya Nkinto,Ruben Mhai, alisema serikali inajitahidi sana kujenga barabara lakini wananchi wanashiriki kuiharibu kutokana na kuswaga makundi ya mifugo barabarani na kusababisha hasara kubwa kwa serikali pamoja na wananchi wanaoishi katika maeneo husika.
Mhai alisema tatizo hili ambalo limekithiri katika Wilaya ya Makalama wenye mifugo wanafanya uharibifu barabara lakini kwasababu hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi yao ndio maana wanaendelea kuharibu miundombinu ya barabara.
Akijibu malalamiko hayo ya madiwani,Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Mkalama Mhandisi Paschal Mafuru alisema ushauri huo wa madiwani utafanyiwa kazi ambapo wataanza operesheni maalum kukamata mifugo inayooitishwa baraba
MWISHO
0 Comments