Header Ads Widget

KIGOMA YAPOKEA VIFAA TIBA VYA RAIS SAMIA

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKOA Kigoma umepokea msaada wa vifaa mbalimbali vya matibabu vilivyotolewa na Raisi Samia Suluhu Hassan ikiwa ni mpango wa kiongozi huyo wa nchi katika kuboresha huduma za afya nchini.


Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari mjini Kigoma alisema kuwa mkoa huo umepokea vifaa vya aina  mbalimbali 53 kwa ajili ya kuimarisha huduma ya afya mkoani humo vikiwa na thamani ya shilingi milioni 214.


Andengenye alisema kuwa vifaa 38  kati ya vifaa 54 vimepokelewa katika kituo cha afya Bunyambo wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma vikiwemo vifaa vya kuimarisha huduma za kujifungua mama wajawazito.


Miongoni mwa vifaa hivyo ni Pamoja na vifaa vya kufanyia upasuaji wa dharula, mashine za usingizi, meza ya kufanyia upasuaji na taa zake, mashine ya kufua na kukausha nguo, vifaa vya kutakasia vifaa tiba, majokofu ya kuhifadhia damu,majokofu ya kutunzia dawa na mashine ya kupima mapigo ya moyo yam toto akiwa tumboni kwa mama mjamzito.



Akizungumzia kupokelewaa kwa vifaa hivyo Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma,Dk. Jesca Leba alisema kuwa vifaa hivyo ni sehemu ya vifaa vilivyotolewa na Raisi Samia kwa mikoa 16 nchini.


Dk.Leba alisema kuwa vifaa hivyo vimepelekwa kituo cha afya Bunyambo wilaya Kibondo kutokana na mahitaji yaliyopo kufuatia kuanza kutoa huduma kwa kituo hicho ambacho ni kipya na hakikuwa na vifaa hivyo.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI