Header Ads Widget

RAIS DKT. MWINYI ASHIRIKI MAZISHI YA BI.FADYA ABDALLA SEIF


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na viongozi na wananchi mbalimbali katika mazishi ya Bi. Fadya Abdalla Seif, aliyefariki dunia leo tarehe 30 Disemba 2025.

Mapema, Rais Dkt. Mwinyi alijumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Jeneza iliyosaliwa Masjid Jamiu Zinjibar, Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Marehemu Bi. Fadya Abdalla Seif ni mama mzazi wa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Ndugu Arif Abdalla Manji. Marehemu amezikwa kijijini kwao Kazole, Mkoa wa Kaskazini Unguja.















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI