Header Ads Widget

JELA MAISHA KWA KUBAKA MWANAFUNZI

Na Fadhili Abdallah, Kigoma

Mahakama ya Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma imemuhukumu Moses Method (23) mkulima na mkazi wa Kijiji cha Kasuga wilayani Kakonko kutumikia kifungo cha Maisha  jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili mwenye umri wa miaka tisa

 

Mbele ya mahakama hiyo Hakimu Mkazi wa mahakama ya wilaya Kakonko, Ambilikile Kyamba alisema kuwa Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka na  ushahidi uliotolewa mahakamani hapo  na upande wa mashitaka na hatimaye kumtia hatiani mshitakiwa kwa kosa hilo.

 

Sambamba na hilo Hakimu huyo wa mahakama ya wilaya ya Kakonko amemuhukumu mshitakiwa huyo  kulipa  fedha taslimu shilingi milioni moja kwa muhanga wa tukio hilo ikiwa ni fidia kwa matendo aliyofanyiwa.

 

Hakimu Kyamba alisema kuwa mahakama hiyo imetoa humumu hiyo kuwa fundisho kwa watu wengine kwani matendo hayo yamekuwa na Atari kubwa kimwili na kiakili kwa watu wanaofanyiwa matendi hayo.

 

Mbele ya mahakama ya wilaya Kakonko Mwendesha Mashitaka Mkaguzi wa Polisi wilaya ya Kakonko, Charles Mwakanyamale alisema kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 17 mwaka jana majira ya jioni katika   Kijiji cha Kasuga Wilaya ya  Kakonko Mkoani Kigoma.

 

 

Mshitakiwa alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 21 baada ya upelelezi kukamilika na kwamba mshitakiwa huyo alikamatwa  akiwa kwenye jitihada za kutoroka.

 

 

Akitoa hukumu hiyo Februari 12,2024 hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kakonko mheshimiwa Ambilikile Kyamba amesema kuwa Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na hatimaye kumtia hatiani mshitakiwa kwa kosa hilo.

 

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI