Header Ads Widget

MZUMBE KUTOA ELIMU YA UWEKEZAJI KWA WASTAAFU.

Na Mbaruku Yusuph Matukio Daima APP, Tanga. 

WASTAAFU wametakiwa kupata elimu ya uwekezaji ili kuweza kutumia pesa zao za kiinua mgongo vizuri badala ya kuanzisha shughuli wasizokuwa na elimu nazo.


Kauli hiyo imetolewa na Dkt Daudi Ndaki Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kilichopo Mkoani Morogoro alipofanya wakati akitoa mafunzo ya kuwaandaa wastaafu na wanaotarajia kustaafu kazi ili kuwaepusha kufanya biashara wasizokuwa na utaalamu nazo.


Aidha Dkt Ndaki alisema Chuo hicho kupitia wataalamu wake wa soko la mtaji kimeanzisha mafunzo hayo takriban miaka minne sasa wakilenga kutoa elimu kwa kundi hilo ili litambue madhara ya kufanya biashara au uwekezaji wasiokuwa na uzoefu nao jambo ambalo limewakumba wastaafu wengi na baadhi yao kupoteza walichokivuna


"Wastaafu wengi wamekuwa wakipata pesa wanakwenda kununua au kuanzisha miradi ambayo hawana utaalamu nayo na kupelekea pesa zile kupotea na hatimae wastaafu hao wanaathirika kisaikolojia"Alisema Dkt Ndaki. 


Dkt Ndaki alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa kutokana na ufahamu na utaalamu waliokuwa nao kwenye soko la mtaji ili kuwafanya wastaafu hao wawe wawekezaji wanatakiwa kuwa na taarifa sahihi ya kitu gani sahihi kipo kwenye soko la uwekezaji.


"Ni jukumu letu kulielekeza kundi hili la Wastaafu namna ya kufanya uwekezaji ki elimu zaidi na kuwawezesha kuona aina ya ujasiriamali ambao wanaweza wakaufanya pindi wamalizapo miaka ya ajira zao"Alisema Dkr Ndaki. 

Hata hivyo Dkt Ndaki alisema Mbinu wanazowapa wastaafu hao zina usimamizi mdogo lakini zina uhakika wa kuendelea kupata kipato baada ya kustaafu kazi zao badala kuzungumzia swala la kikokotoo vibaya na huku kunatokana na kutokuwa na elimu ya uwekezaji. 


Alisema ni jambo la kawaida kwa Watanzania kupata elimu ya uwekezaji na mipango ya fedha baada ya kustaafu na huo ndio uhalisia unaonyesha watu wengi wanakuwa na ufahamu mdogo wa masuala ya biashara,ujasiriamali,uwekezaji n.k.


Alizungumzia suala la kikokotoo na kusema kuwa watumishi wengi wanaamini kupata kiwango kikubwa cha pesa ndio tija kwao badala ya kupata elimu ya uwekezaji na wote ni mashuhuda wastaafu wanapata pesa nyingi lakini baada ya muda mfupi pesa hizo zinaisha.


Dkt Ndaki ambae ni mtaalam wa mipango mkakati ya fedha na uwekezaji kwa watu ambao wanajiandaa kustaafu toka Chuo Kikuu cha Mzumbe aliongeza kusema kuwa Jukumu lao ni kuwaelekeza wastaafu hao namna ya kufanya uwekezaji kielimu zaidi mfano katika suala la hati fungani,uwekezaji kwenye mifuko ya uwekezaji ya pamoja na uwekezaji kwenye soko la mtaji la Jijini Dar na maeneo mengine ndani na hata nje ya Nchi.


Akizungumza na mwandishi wa Matukio Daima Blog Huda magala ambae alikuwa mfanyakazi katika Hospitali ya Mkoa Morogoro MRRH ambae amestaafu Feb 2 mwaka huu alisema lengo la kuhudhuria mafunzo hayo ni kupata elimu ili iweze kuwasaidia baada ya kupata pesa za kiinua mgongo ili ajue namna ya kuzitunza au kuwekeza katika biashara itakayoifanya pesa zake ziendelee kubaki salama.

Huda alisema mafunzo hayo ni mazuri na yanapaswa yawahusu wastaafu wote Nchini ili yaweze kuwa na tija kwa maisha yao baada ya kustaafu kazi hasa kwa 

kundi hilo ambalo bado halijakuwa na elimu hiyo ambayo ndio mkombozi kwao.


Kwa upande wake Richard Leiser ambae ni mfanyakazi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Jijini Arusha ambae anategemea kustaafu miezi 11 ijayo alisema elimu hiyo ndio mkombozi kwao na imewafumbua macho wastaafu hao ambao kwa sasa wanahisi wanakwenda kuwa wawekezaji wazuri.


Mafunzo hayo ambayo yanafanyika Jijini hapa yameanza Feb 9 na yanatarajiwa kumalizika Feb 16 mwaka huu ambapo yamewashirikisha watumishi wa Serikali toka Mikoa mbalimbali hapa Nchini. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI