Header Ads Widget

FUNGA FUNGA KWA WAFANYA BIASHARA IWE MWISHO SASA.




Na Shemsa Mussa,Kagera 

Mstahiki Meya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Gypson Godson amepiga marufuku watoza ushuru ndani ya Manispaa hiyo kufunga maduka ya wafanyabiashara badala yake wajikite kwenye kutoa elimu zaidi  ili wafanya Biashara hao waelimike na kulipa Kodi kwa hiyali yao.


Akizungumza wakati wa kuhitimisha kikoa cha Baraza la Madiwani Manispaa hiyo wakati wa kupitisha bajeti katika mwaka wa fedha 2024/2025 alisema elimu iendelee kutolewa kwa wananchi na wafanya Biashara kwa ujumla hata kwa kutumia vyombo vya habari namna ya kulipa na kukusanya Kodi.


Godson ameendelea kusema kuwa Halmashauri hiyo iwaite wafanya Biashara wote wanaodaiwa na Halmashauri hiyo wazungumze nao na watakao kaidi kulipa wafikishwe Mahakamani kama sheria inavyo elekeza.


Hata hivyo Ajesy Katumwa ambaye ni Afisa Tawala wilaya Bukoba akitoa salamu za serikali kwenye baraza hilo kwa niaba ya mkuu wa wilaya Bukoba Erasto Sima amesema Halmashari hiyo inaendelea kutoa elimu ya Mapato ili wananchi wazidi kupata uelewa wa kulipa kodi kuliko kutumia mabavu.


Awali akisoma taarifa ya mapendekezo ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025  Kaimu Mkurugenzi Helleni Rocky amesema jumla bilioni 32.6 zimetengwa kwa ajiri ya shughuli mbalimbali za maendeleo kwanye Manispaa hiyo kwa vipaumbele ikiwemo kuinua Uchumi wa Manispaa hiyo ,Ujenzi wa soko la dagaa kastam, Ujenzi wa maduka eneo la kishenge, ukusanayaji wa mapato na kuweka mikakati ya kutambua na kuongeza vyanzo vipya vya mapato.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI