Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP Njombe
Naibu waziri mkuu na Waziri wa Nishati Dokta Dotto Biteko amesema wanaendelea kuchukua hatua kwa watendaji wa Tanesco wanaokwamisha jitihada za kuwapelekea wananchi umeme.
Dokta Biteko ametoa kauli hiyo akiwa katika kijiji cha Ikwavila kata ya Kijombe Wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe baada ya kuzindua umeme wa Rea katika shule ya msingi Ikwavila na kwamba ucheleweshwaji wa kupeleka Transfoma kubadili zinazoungua na kusababisha malalamiko ataendelea kuchukua hatua.
Mbunge wa jimbo la Wanging'ombe Naibu waziri Tamisemi Dokta Festo Dugange amesema Vijiji vyote 108 vimepata umeme wa Rea bado vitongoji 158 japo kuna changamoto ya upungufu wa umeme huo.
Mhandisi Geofrey Chibulunje Mwakilishi wa mkurugenzi mkuu REA katika taarifa yake amesema Mkoa wa Njombe Vijiji 20 pekee na vitongoji 668 ndivyo havijapata umeme na kazi inaendelea.
Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Claudia Kitta anasema vitongoji 72 vinaendelea kuunganishwa umeme wa Rea hivyo wanatarajia kupitia ujio wa Naibu waziri mkuu kasi itaongezeka.
Naye Mbunge wa Jimbo la Wanging'ombe Dokta Festo Dugange ambaye ni Naibu waziri wa Tamisemi amesema Wilaya yake yenye vijiji 108 vimepata umeme wa REA na kwamba jitihada mbalimbalimbali zinaendelea ili kupeleka kwenye vitongoji.
Wananchi wa Ikwavila akiwemo Eliza Mdapo na Syrivester Kigola Diwani wa kata ya Kijombe wamepongeza hatua ya serikali kuwasha umeme katika vijiji vyote vya kata hiyo huku wakiomba kusaidiwa hadi kwenye vitongoji vingine.
0 Comments