Header Ads Widget

BREAKING:MWANDISHI KAZIMBAYA MAKWEGA AKAMATWA NA POLISI

      C E.O wa Mwanakwetu Blog  Makwega 

Ndugu waaandishi wenzangu muda huu nimefika kituo kikuu cha polisi kati na mawakili wa wawili wa OJADACT kufuatilia kukamatwa kwa Mwandishi  wa habari kazimbaya makwega.


Kwa bahati nzuri tumemkuta  hapa kituoni na nimepata nafasi ya kuongea naye ana kwa ana kama dakika 5 hivi.


Wakati naongea naye wakaja maafisa waliojitambulisha kuwa wanatoka ofisi ya RCO Dodoma na wamekuja kumchukua ili waondoke naye.

Makwega Katika picha na spika Dkt Tulia 

Nao pia walikubali kuongea na mimi pia na sio mawakili nami nikafanya hivyo tukaongea na wakaniambia wanaondoka naye kwenda dodoma saa 7 mchana.


Pia wakasema kuna tuhuma huko Dodoma za kujibu hivyo tuwe na amani kwani hizo ni tuhuma.


Hapo nikawauliza kuwa  kama.wanatoka Dodoma mbona tumeongea na ofisi ya RPC dodoma na ikathibitisha kuwa hakuna askari wake waliokuja Mwanza.


Wao wakajibu kuwa ofisi ya RPC ni kubwa ila wao wanatoka ofisi ya RCO Dodoma.


Maelezo toka kwa makwega mwenyewe ni kuwa alikamatwa jana kwao Malya na akanyang'anywa laptop na simu zake tatu na pia alipofika hapa kituoni akaandikishwa maelezo.


Gari yenye namba za usajili SU 45605 landCruiser imeondoka na Makwega hapa kituo cha polisi kati Mwanza.


Maelezo ya mwisho toka kwa watu wanaomshikilia walisema wataondoka saa 7 mchana ila kwa sasa wanaenda wapi ? Hatujajua na ilikuwa ngumu kuhojji.


 Afya ya Makwega 

Ipo salama kabisa nilipoomba  tumpe kwanza chai anywe wakasema watampa wao na hiyo ni haki yake kama binadamu hivyo watamhudumia.


Naomba wemzetu mlioko Dodoma jipangeni kwa ajili ya kumpokea .


 Ushirikiano na Jeshi la polisi.

Tangia nilipofika kituoni nimepata ushirikiano mzuri na nilipojitambulisha wakamruhusu niongee naye kwa kina.


Ahsanteni sana wote


 Edwin Soko 

 Mwenyekiti

 OJADACT 

 MPC

Post a Comment

1 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS