IMEELEZWA kuwa Wastani wa asilimia 80 ya Kina mama katika Mkoa wa Kaskazini Unguja na Pemba wanakabiliwa na tatizo la Lishe linalopelekea kukithiri wa vifo na mama na Mtoto wakati wa kujifungua.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Kinga kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Salim Nassor Slim wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea kambi ya matibabu itakayofanyika Mkoa wa Kaskazini Unguja Machi 04 hadi 08 mwaka huu na kuendeshwa na Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation.
Dkt. Salim Slim amesema kuwa, Tatizo la Lishe kwa kina mama ni kubwa Visiwani Zanzibar ambapo asilimia 80 ya Wanawake katika Mkoa ws Kaskazini Unguna na Pemba wanakabiliwa nalo huku asilimia 48 kwa Zanzibar nzima.
"Watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na maradhi yasiyoambukizwa kutokana na kutokuwepo kwa Lishe bora ambapo husababisha Vifo vya kina mama na Watoto hasa wakati wa kujifungua," amesema.
"Tuendelee kuhamasisha Lishe bora kwa Wakina mama maana madhara yake ni makubwa katika jamii na maradhi yanaongezeka na tatizo la Kuzaliwa Watoto wenye changamoto mbalimbali linaongezeka.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Maisha Bora Foundation Fatma Fumbo amesema kuwa kutokaba na changamoto za kinamama Taasisi hiyo imejipanga kuonesha Kambi ya Matababu kwa siku Tano kuanzia 04 hadi 08 katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema kambi hizo zitakuwa endelevu katika Mikoa yote ya Zanzibar na wamejipanga kuwafikia Wananchi zaidi ya Elfu 20.
"Sisi maisha bora Foundation tumejikita katika mambo Watatu, Uchumi wa Buluu, Kuimarisha Afya za kina mama na kupambana na udhalilishaji na Ukatili wa kijinsia na sasa tunaanza na utoaji wa Huduma za Afya," amefafanua.
Mapema Daktari Dhamana wa Wilaya Kaskazini A Unguja, Dk. Humid Juma Said amesema kuwa, Kambi hiyo zitahusisha Matibabu na uchunguzi kwa maradhi mbalimbali.
0 Comments