Header Ads Widget

TMA YATOA TAHADHARI MSIMU WA MASIKA

Na fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imetoa mwelekeo wa mvua za masika kwa msimu wa mwezi Machi hadi Mei kwa mwaka 2024 ambapo mvua zinatarajiwa kuwa wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt Ladslaus Chang'a amesema kuwa mvua za masika zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi febuari 2024 katika maeneo mengi, huku ongezeko la mvua likitarajiwa katika kipindi cha mwezi Machi 2024.


"katika maeneo mengi mvua  zinatarajiwa kuisha katika wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei 2024 katika maeneo mengi, huku miongoni mwa athari zinazotarajiwa kutokea ni pamoja na magonjwa ya mlipuko kutokana na uchafuzi wa maji, kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kuongezeka na vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo"amesema Dkt Chang'a.


Aidha amesema mvua za Masika ni mahsusi kwa maeneo ya nyanda za juu Kaskazini Mashariki ( mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro), Pwani ya Kaskazini ( Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, mikoa ya Pwani ikijunuisha visiwa vya Mafia, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba), ukanda wa ziwa Victoria (mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara pamoja na Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.


Hata hivyo, amesema mifumo ya hali ya hewa joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la magharibi mwa bahari ya Hindi (Pwani ya Afrika Mashariki) ikilinganishwa na upande wa Mashariki mwa bahari ya Hindi huku joto la bahari la chini kidogo ya wastani linatarajiwa katika eneo ya kusini mwa kisiwa Cha Madagaska.


Sambamba na hayo amesema kutoka na hali hiyo wakulima wameshauriwa kuandaa mashamba, kupanda na kupalilia na kutumia pembejeo husika Kwa wakati, kutumia mbinu bora na teknolojia za kuzuia Maji kutuama shambani, mmomonyoko na upotevu wa rutuba na kuchagua mbegu na mazao sahihi Kwa ajili ya msimu huu wa Masika.


Hata hivyo ametoa wito kwa Menejimenti za maafa kuwa vipindi vya mvua kubwa vinaweza kujitokeza na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi na kupelekea uharibifu wa miundombinu, mazingira, upotevu wa mali na maisha hivyo mamlaka husika ziendelee kuratibu utekelezaji wa mipango ya kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS