NA THABIT MADAI,ZANZIBAR BENKI Kuu ya Tanzania imetoa wito kwa jamii kuwa na muamko wa kusajili vikundi vya kuweka na kukopeshana Fedha katika maeneo mbalimbali nchini ili kuepuka hasara ambazo zinazoweza kupatikana wakiwa wanasimamia vikundi vyao kienyeji.Wito huo umetolewa na Afisa Mkuu Mwandamizi kutoka Idara ya Usimamizi wa huduma ndogo za Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Deogratias Mnyamani katika siku ya pili ya mafunzo kwa Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari yanaondeshwa katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya BoT Zanzibar.Amesema kwamba, Kuna faida nyingi za kusajili vikundi ikiwemo kutambulika rasmi kisheria sambamba na usalama wa Fedha za Wanachama unakuwa Mkubwa zaidi."Unaposajili hivi vikundi vya kuweka na kukopeshana fedha zinakuwa katika usalama Mkubwa zaidi wa fedha za Wananchama na hata Kesi zinapungua katika jamii yetu," ameeleza."Nichukue nafasi hii kuwashauri wote ambao wamejiunga katika vikundi ambavyo havijasajiliwa wajitokeze kusajili ili kupata faida zaidi," ameongeza.Katika hatua nyingine ameomba Waandishi wa Habari kuendelea kutoa Elimu kwa jamii juu ya kusajili vikundi vya kukopeshana fedha ili kuokoa hasara ambayo wanajamii wanaweza kuipata."Tunategemea kuwa nyinyi Waandishi wa Habari mutaendelea kutoaelimu kwa jamii ili kuepuka hasara ambayo inaweza kujitokeza,"Ameeleza.






0 Comments