Header Ads Widget

KAMANDA WA POLISI AKABIDHI SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI WENYE UHITAJI

 


Na Ibrahim Yassin Matukio App Songwe


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP. THEOPISTA MALLYA akikabidhi sare za shule kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wa shule ya Msingi Katete iliyopo kata ya Mpemba Mjini Tunduma Mkoani Songwe leo Tarehe 23 Februari 2024 SCP Mallya amekabidhi sare hizo alipotembelea shule hiyo na kuwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili wawe wataalamu wa fani mbalimbali watakaotegemewa katika shughuli za maendeleo ya Taifa letu.Mmoja wa wanafunzi waliopatiwa Msaada huo ambaye hakujitambilisha jina amesema msaada huo utainua hali ya kujisomea huku akimuahidi mkuu huyo ufaulu mzuri. Mkuu huyo wa polisi amekuwa na kawaida hiyo ya kusaidia watoto wenye uhitaji maalum katika nyanja mbalimbali.Post a Comment

0 CommentsMAGAZETIBBC NEWS