Chama cha riadha mkoa wa Kilimanjaro kimesema kutokana na kuwepo mashindano mbalimbali yanahusisha mchezo wa riadha katika mkoa huo imekuwa sababu ya wakazi wa Kilimanjaro kuhamasiki kujiunga na mchezo huo.
Akiwa katika uzinduzi wa mbio za kili marathon yaliyofanyika katika hoteli ya Salsalnero iliyopo mjini Moshi mwenyekiti wa Riadha mkoa wa Kilimanjaro Abraham mikumi ameeleza kuwepo kwa mchezo wa riadha katika mashindano na matamasha ya kimichezo kulivyoinyanyua mchezo huo katika mkoa huu.
Akizungumza katika uzinduzi wa mbio hizo za Kilimanjaro premium lager half marathon zinazotarajiwa kufanyika uwanja wa chuo kikuu ushirika moshi mkoani Kilimanjaro katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro TIXON NZUNDA anasema licha ya mchezo wa riadha kuwa na muamko pia imekuwa chachu ya kukua kwa utalii wa kimichezo.
Nao baadhi ya washiriki ambao ni wadau wa hoteli ya salsalnero wamewashukuru wadau wa kili marathon kwa kuwaamini na kusema wataendelea kutoa huduma Bora ambayo itakayowawavutia watu Mbalimbali.
Hata hivyo washiriki takribani elfu 12 wanatarajiwa kushiriki mbio za Kilimanjaro premium lager intenation Marathon huku msindi wa kwanza wa mbio hizo kwa upande wa wanaume na wanawake wanatarajiwa kupata zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 4.
0 Comments