Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Losirwa kata ya Moshono wanaodai fidia zao wakisikiliza jambo kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Arusha Timoth Sanga
NA NAMNYAKI KIVUYO, ARUSHA.
Zaidi ya Wananchi 60 wa jiji la Arusha kata Moshono mtaa wa Losirwa wamekiomba chama cha Mapinduzi (CCM) kuwasaidia kupata fidia zao kwa wakati katika suala zima la kulipisha jeshi la wananchi (JWTZ) katika maeneo yao jambo lilidumu kwa muda mrefu huku wakishindwa kufanya shughuli zozote za maendeleo kutokana na zuio walilopewa.
Wananchi hao wametoa ombi hilo wakati katibu wa CCM wilaya ya Arusha Timoth Sanga alipotembelea kata hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembele mitaa yote 154 katika kata 20 za jiji la Arusha ambapo walisema kuwa wameshafanyiwa tathimini na Jeshi hilo na baadae ofisi ya hazina lakini wanashanga ni jambo gani linalozuia kulipwa fidia hizo.
Madina Hamisi mmoja wa wananchi hao alieleza kuwa yeye ana familia na wakati wanapewa zuio la kutokufanya maendeleo yoyote katika eneo hilo alikiwa amejenga chumba kimoja na sebule ambapo kwa sasa watoto wake ni wakubwa wako shule za sekondari ni wa jinsia tofauti lakini kutokana na zuio hilo watoto wale bila kujali jinsia wote wanalala sebuleni.
“Imagine mimi hapa niko chumbani alafu mtoto wa kike na wa kiume wako wamelala sebuleni, ni kitu ambacho kinaniumiza kwasababu ningeshaendeleza ujenzi watoto wa kiume wangukuwa na sehemu yao ya kulala lakini pia wa kike lakini nina stop order na sasa ni miaka watoto wanalala kama vile watoto wa mbwa,”Alisema Madina.
“Ninaomba waheshimiwa mtusaidie pesa ipatikane kwa wakati, tuliwachagua tunajua mnaweza tusaidieni ili na sisi tuweze kutoka hapa na kwenda kufanya maendeleo tumekaa hatuelewi chochote ni kama Dunia imesimama kwetu,”Alieleza.
Masamaki Mollel Chama chochote ambacho kinaunda Dola kina nguvu na ndicho kilichowaweka viongozi madarakani na tunajua chama hakina shida bali watendaji hivyo wanatarajia kupata majibu ya changamoto hiyo ili waweze kusonga mbele.
“Chama chetu hakina shida lakini watendaji ndio chanagamoto kwa maeneo haya yameshafanyiwa tathimini tunasema miezi sita lakini ni mwaka kwasabu ya siku ambayo mtathimini mkuu alipoweka saini miezi hiyo mingine inakuwa ya mchakato,” Alisema.
“Wanajeshi wanalima na kwa chama chetu sikivu serikali na Rais wetu sisi wote tunapinga umasikini na pia ni slogani ya baba wa taifa lakini leo hii sisi tunakufa njaa na wanajeshi wanalima mpaka nje na sisi tunasema kwa maamuzi ya mtu mmoja mmoja mimi nikiwemo mwaka huu nitalima eneo langu nipigiwe risasi pale pale kwasabubu sijalipwa hela,” Alisema Masamaki.
Mselemaya Lemeite alisema kuwa wanasikitika kwani hawaruhusiwi kufanya chochote hata kulima mashamba yao hali inayopelekea kukumbwa na janga la njaa ambapo wametembelewa mwezi wa tatu na kuhaidiwa hadi mwezi wa nane watakuwa wameshalipwa lakini hawakutokea na baade walirudi kuhakiki mwezi wa 11 na kuambiwa mwezi wa 12 malipo yao yatakuwa tayari na wamewasubiri mpaka leo hawajatokea.
“Hatujui hata tunafanya nini manake familia zetu zinalala njaa kwani mashamba ambayo tulikuwa tunayategemea kwa uzalishaji haturuhusiwi kulima na jeshi, sasa kwanini malipo yetu yanachelewa hivi?, lakini pia tunajiuliza kwanini tuambiwe tunapewa hela badala ya kupewa ardhi nyingine kama fidia,” Alisema mzee Lemeite.
Akiwajibu wananchi hao katibu wa CCM Wilaya ya Arusha mjini Timoth Sanga alisema kuwa amelichukua jambo hilo kwa uzito wake na kuahidi kulifuatilia kwani hapendezwi na kuona akina mama wakilia na wazee wakihangaika huku serikali yao inayoongozwa na chama hicho kikiwepo ambapo atarudi baada ya siku saba katika eneo hilo kupeleka majibu kwa wananchi hao.
Aidha wakati huo huo Katibu huyo aliweza kulifuatilia jambo hilo kwa kuongea na Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa kwa njia ya simu na kusema kuwa muda wowote kuanzia sasa wananchi hao watalipwa kwani kwenye ofisi yake jambo hilo lilishashughulikiwa tangu mwezi wa 11,2023 na atawasiliana na wanaohusika ili kuweza kulisukuma.
0 Comments