Na WILLIUM PAUL.
WAJUMBE wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wametembelea mashamba ya miwa ya Mkulazi (Wilaya ya Kilosa) na Mtibwa (Wilaya ya Mvomero) na viwanda vyake vya sukari ambapo Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ni mjumbe wa kamati hiyo.
Ziara hiyo ilikuwa mahsusi kufuatilia uzalishaji wa sukari kwenye viwanda hivyo katika kipindi hiki cha mvua za El Nino zinazoendelea nchini.
Wajumbe wa kamati walijionea uharibifu mkubwa wa miundombinu uliosababishwa na mvua na kuzorotesha uzalishaji wa Sukari na kupata fursa ya kuishauri Serikali.
Mwisho
0 Comments