MTAKATIFU , Mtakatifu Mungu Mwenye Nguvu Kwa neema na nguvu yako tumeamka salama.
Asubuhi hii tumekuja mbele yako kukushukuru wewe Mungu na kuomba ulinzi na Baraka Zako siku nzima ya leo.
Tunaomba shusha uponyaji wako Kwa wagonjwa,neema na Baraka Kwa wote hapa kundini siku hii ya Leo Kila mmoja apokee Baraka Zako kwenye Kila hatua atakayopitia,ulinzi wako papote tuendapo.
Mungu tunawaweka mikononi mwako wahubiri wote wa watakaosimama kutulisha Neno lako la kweli siku hii ya Leo huku tukiomba tuepushe na wote wanaotumia vibaya Neno lako Kwa mahubiri yasiyo faa.
Maana imeandikwa Katika zaburi 12:6
Kuwa
Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa karibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.
Hivyo tunaamini Katika maandiko yako matatifu na asiwepo wa kwenda kinyume na maandiko yako hata kuifinyanga injili ili kujipatia pesa .
Hivyo tunaamini kupitia kitabu za Zaburi 13:5 Nami nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.
Hakika Mungu siku hii ya Leo nikiamini nitatembea nawe na Kamwe asiwepo wa kuniyumbisha .
Mikononi mwako nawaweka Viongozi wa Taifa hili wakiongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na wote wenye mamlaka uwape Afya njema nao watuongoze kadri vile utakavyo Mungu na si Kwa mapenzi yako.
Kwa kuwa wewe Mungu ni Mungu Mwenye Nguvu nimeomba haya Kwa imami nikiamini hakuna Mungu zaidi yako wewe.
AMEN
0 Comments