KATIKA kuadhimisha sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar ,taasisi ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mkoa wa Pwani imetoa msaada Kwa wafungwa wa gereza la Ulete Rufiji.
Akizungumza wakati wa kumkabidhi msaada huo kwenye Gereza la Utete Katibu wa Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoa wa Pwani Omary Punzi kwaniba ya Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Taifa Mheshimiwa Paul Petro Kimiti na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi hiyo Mheshimiwa
Mizengo Peter Pinda (Waziri Mkuu Mstafu) Kwa kutoka Msaada wa Sabuni za unga na Vipande,Mafuta ya Kupakaa,Miswaki na Dawa Meno Pamoja na Juisi Katika Gereza hilo.
Amesema Misaada hiyo ilikuwa inalenga Kusherekea Miaka 60 ya Mapinduzi Tukufu ya Zanzibar Tarehe 12.1.2024 Kwa kuwalenga wafungwa na kuwaomba Wadau nchini wajitokeze Kwa wingi kuwasaidia Wafungwa na mahabusu magerezani Kwa Kutoa misaada mbalimbali kwani bado wanamahitaji mengi.
Kwa Upande wa Mkuu wa Gereza la Utete Christopher Mwenda Kwa niaba ya MKUU WA magereza Mkoa amewashukuru Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoa wa Pwani namna wanavyoendelea kuwatia moyo wafungwa siyo mara ya kwanza Taasisi hiyo kupeleka Msaada Mwaka Jana walipokea cartoon za Box 50 za Taulo za kike Kwa ajili ya Wafungwa wanawake gerezani hapo.
Aidha ameomba Wadau wajitokeze Kwa wingi kuwasaidia Wafungwa Bado wanahitaji mahitaji mengi Serikali Haiwezi kufanya peke yake katika mahitaji.
Naye Monica Mbilla Mkuu wa idara ya Malezi ya Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoa wa Pwani amesema Msaada Mkubwa atakao wasaidia kuhakikisha wanapewa elimu na Msaada wa kisheria.
++++
0 Comments