Header Ads Widget

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA WERUWERU - MANUSHI - KOMBO KATIKA KATA YA KIBOSHO MAGHARIBI



NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


MBUNGE wa Jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi amekagua ujenzi wa barabara ya Weruweru- Manushi - Kombo yenye urefu wa kilomita 10.2 ilipoyo katika bajeti ya 2023/2024 katika Kata ya Kibosho Magharibi.


Katika ziara hiyo Mbunge aliambatana na Diwani wa kata hiyo Prosper Emili Massawe, na Diwani wa viti maalumu Fabiola Massawe pamoja na wataalamu kutoka TARURA na viongozi wa CCM Kata na wananchi.



Katika ziara hiyo Injinia Mchanga kutoka  TARURA wilayani Moshi alitoa taarifa kwa niaba ya Meneja wa TARURA wilaya na kusema kuwa barabara hiyo imetengewa kiasi cha shilingi milioni 250, na mpaka hivi sasa wameshapokea kiasi cha shilingi Milioni 135,642,000 ambacho ndicho mkandarasi atalipwa.


Aliendelea kusema kuwa mipango ni kufungua barabara yote kilomita 10.2 na kwa mwaka huu wa fedha Moramu itawekwa kwenye kipande cha kilomita 3 na kalvati 6.



Akiongea kwenye ukaguzi huo, Mbunge Ndakidemi alitoa wito kwa TARURA kuweka mifereji ya kuchepusha maji kutoka barabarani kwani  hiyo ndiyo suluhu ya kukinga barabara isiharibike mapema. 


Aliwaomba wananchi wasaidiane na TARURA kuhakikisha maji hayasimami katikati ya barabara na kumuomba Mkandarasi kufanya kazi kwa viwango na kuimaliza kazi kwa wakati kwani wananchi wanasubiri kuona matokeo.



Mkandarasi aliyepewa zabuni hiyo ni Brand Mark Contractor Ltd ambapo wanatagemea kukabidhi mradi huo kufikia tarehe 02/06/2024. 



Diwani wa Kata hiyo Prospa Massawe na wananchi waliohojiwa kwa nyakati tofauti walimshukuru Mbunge kwa ufuatiliaji pamoja na kuishukuru Serikali kwa kuikumbuka barabara hiyo ambayo haijafanyiwa ukarabati wa aina hiyo kwa kipindi kirefu.

Mwisho.. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI