Header Ads Widget

SERIKALI YAPOKEA MAONI KWA WANANCHI KUHUSU MASUALA YA KITAIFA

Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imesema inatambua umuhimu wa wananchi kushiriki katika maamuzi yanayohusu masuala ya kitaifa na kimataifa ikiwemo utoaji wa maoni kuhusu marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001.


Kauli hiyo imetolewa jijini  Dar es Salaam, na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba wakati akifungua kongamano la kukusanya maoni ya wadau mahsusi kuhusu mapendekezo na marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka .


Aidha amesema ndani ya kongamano hilo wadau hao watapata fursa adhim ya kuelewa kwa kina masuala muhimu yaliyomo katika sera ya mambo ya nje ikiwemo misingi ya sera zao na malengo yake.

”Pia wataweza kupata uelewa wa historia ya sera ya mambo ya nje tangu uhuru hadi 2001 ambapo utekelezaji wa sera kuanzia mwaka 2001 hadi sasa mapitio ya sera hiyo,”amesema.


Amesema kuwa,  kuna umuhimu wa wadau mbalimbali kiwemo wanasiasa asasi za kiraia viongozi wa dini kushirikishwa wa kutoa maoni yao mahsusi katika mchakato wa marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001.


"Tanzania kama yalivyo mataifa mengine,ambayo nchi zao zinavyokabiliwa na fursa na changamoto katika ushiriki wake kwenye jukwaa ya kimataifa, ni vema kuwa na sera madhubuti ambayo ni muhimu katika kutumia ipasavyo fursa hizo na kukabiliana na changamoto ambazo zitajitokeza,”amesema Waziri Makamba maendeleo endelevu na mustaksbali wa taifa pasipo kuathiri wananchi wake.

Hata hivyo, amesema katika kongamano hilo,wizara yake inapenda kusikia kutoka kwa wadau jinsi wanavyoona marekebisho yaliyofanyika katika sera na ni maoni gani waliokuwa nayo kuhusu njia zitakazochukuliwa kufikia malengo wanayotamani kufikia.


Naye, mongoni mwa Viongozi wa Kisiasa waliohudhuria kutoka chama cha wananchi Cuf Profesa Ibrahim Lipumba amesema wanaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwani imekuwa sikivu sana haiwezi kuamua chochote bila kuwashirikisha wananchi wake watoe maoni yao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI