Header Ads Widget

MWENYEKITI WA BODI RUWASA ARIDHISWA NA KASI YA UJENZI WA MRADI WA MAJI NYANGAO - RUANGWA

NA HADIJA OMARY

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA Mhandisi Ruth Koya ameonyesha kulidhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa maji Nyangao Ruangwa  unaotekelezwa na Mkandarasi Emirate Builders Compan limited  kwa gharama ya shilingi bilioni 119.

Akiwa Ziarani Mkoani Lindi katika kukagua Miradi ya maji inayotekelezwa na RUWASA Mkoani humo  jana 

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo amefurahishwa kuona maendeleo ni mazuri na mkandarasi bado yupo katika eneo la kazi.

Amesema Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza hii miradi ya maji kwa madhumuni makubwa ya kusogeza huduma karibu na wananchi ikiwa pamoja na kutekeleza kauli mbiu ya kumtua mama Ndoo kichwani.


Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Lindi Mhandisi Muhibu Lubasa amesema mradi huo utakapokamilika utanufaisha vijiji 55 kutoka Wilaya ya Lindi,  Ruangwa na Nachingwea  ambapo mpaka sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 18 na unatarajiwa kukamilika mwezi July mwaka 2025.

"Kwa ujumla mradi huo umefikia asilimia 18 ya utekelezaji wake sisi kama wasimamizi tumeridhishwa kuwa mkandarasi anaweza kuendelea na mradi huu na kuukamilisha kwa wakati uliopangwa" Mhandisi Lubasa .

Saidi Msangi  Meneja miradi wa kampuni amesema wamejipanga  kuhakikisha tunakamilisha mradi huu kwa muda uliopangwa ambapo shughuli zote zinazotakiwa kufanywa hufanyika kwa wakati mmoja.

" kama mlivyojionea wakati hili tank linaendelea kujengwa tayari tumeshalaza mabomba katika maeneo mbali mbali kwa ajili ya kuanza kutoa maji kwenye chanzo ambapo pia tayari tumeshajenga vituo viwili vya kusukuma maji na uwenda kama mambo yataenda vzuri mradi unaweza kukamili mwezi wa nne au wata tano  2025 kabla ya muda uliopangwa wa mwezi wa saba 2025"



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI