Header Ads Widget

MSEMAJI WA SERIKALI WAKURUGENZI SHIRIKISHENI WAANDISHI WA HABARI KUISEMEA MIRADI

Na Matukio Daima Media, Mbeya

MSEMAJI mkuu wa serikali,Mobhare Matinyi  amewataka wakurugenzi wote nchini kushirikisha waandishi wa habari na maafisa habari katika kutembelea miradi ya Maendeleo pamoja na kuandaa mikutano ya hadhara na kuitolea taarifa.


Matinyi amesema hayo leo wakati wa mkutano na wakurugenzi wa halmashauri saba za  mkoa wa Mbeya pamoja na waandishi wa habari  ambapo lengo kuu la mkutano huo ni kueleza mafanikio katika utekelezaji wa miradi ya  maendeleo.


Amesema kuwa kwa kazi kubwa inayofanywa na wakurugenzi wa halmashauri nchini ni muda  muafaka kwao kuwa pamoja na waandishi wa habari na maafisa habari ili taarifa za kazi ziweze kufika kwa wananchi .


"Katika ngazi ya Mkoa taarifa huwa zinafika kwasababu  ni Mkoa ambao upo  katika Mji mkubwa na moja miji katika nchi  yetu kuna vyombo vya habari vya kutosha hivyo”amesema.


Ameongeza kuwa ” Hakikisheni  mnakuwa karibu na vyombo vya habari  andaeni  mikutano na kutoa taarifa za miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali na kufanya ziara maalum kutembelea miradi na hiyo ndo itakuwa njia bora  ya  watanzania kujua  nini serikali ya awamu ya sita  inafanya "amesema Msemaji mkuu wa serikali.


Hata hivyo Matinyi  amesema Mkoa wa Mbeya  wa kimkakati katika nchi   umekuwa ukipokea wafanyabiashara wa nchi nne ambazo ni , Malawi,Zambia,Congo pamoja na Zimbabwe huku alisema Mkoa wa Mbeya  umefanya vizuri katika mazao ya biashara na upatikanaji wa madini ya  dhahabu  kutoka kilo 20 mpaka 300.



Awali akizungumzia kuhusu wanafunzi walioripoti Shule,Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amesemampaka sasa wanafunzi walioripoti shule kuanza kidato cha kwanza ni asilimia 80,huku waliokatisha  masomo zaidi ya 500 wamerudi shule kuendelea na masomo  ili waweze kutimiza ndoto  zao.


Aidha mkuu huyo wa mkoa amezungumzia kuhusu mapato ya mkoa na kusema kuwa wamekusanya zaidi ya Bil.36.7 kati ya Bil .49 ambazo wilaya za Chunya,Busokelo na Rungwe zinaongoza kwa makusanyo ya mapato.


Missana Kwangura ni mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya Mbarali amesema kuwa kwa miaka mitatu wamepokea zaidi ya Bil.90 .


Kwangura amesema kuwa sekta ya  elimu msingi walipokea Bl.3.4 na  kuwa shule  za Msingi 139  na kuwa ndani ya miaka mitatu wameweza kuongeza shule 13 na hivyo kufikia shule 142 za msingi.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI