Header Ads Widget

DCEA :KUTOA ELIMU KWA JAMII DHIDI YA MADHARA YA DAWA ZA KULEVYA

Na Hamida Ramadhani Matukio Daima app Dodoma

KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya(DCEA) ,Aretas Lyimo amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wazazi,viongozi wa dini na jamii kwa ujumla kushirikiana katika kuhakikisha kwamba watoto na familia kwa ujumla hawaingii katika matumizi ya dawa za kulevya


Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wao katika wiki ya sheria nchini ambapo amesema kutokana na Oparesheni mbalimbali wanazoendelea kufanya wamebaini watoto hasa waliocha shule na wanaotelekezwa mitaani ndiyo wengi wanaotumika katika usafirishaji wa dawa za kulevya nchini na maeneo mbalimbali.


Vilevile amesema wanaendelea kubaini mitandao ya dawa za kulevya za heroine,kokeini pamoja na methamphetamine pamoja na wale wakulima wakubwa wa mashambani wenye bangi pamoja na mirungi 

"Tumebaini wengi wao pia wanafanya hii biashara kwa rimoti  wao wenyewe hawafanyi hiyo biashara wanawatumia watu wengine na wote tumeshawatambua na tunayoorodha yao na wale wanaotumiwa pia tunayo orodha yao, " Amesema


Na kuongeza "Unaendelea kufanya oparesheni tutaendelea kuwakamata lakini kuanzia sasa hivi tutawaunganisha pia na hao wanaofanya biashara kwa rimoti tunawajua na wengine wanabiashara zao kubwa tutahakikisha kwamba tuwaonye waache hiyo biashara mwisho wa siku tutawakamata ,"


"Kwahiyo wahakikishe wanaacha hiyo biashara watafute biashara halali za kufanya ili tulijenge taifa letu tujenge uchumi wetu tujenge ustawi wa jamii kuhakikisha kwamba biashara ya dawa za kulevya nchini inaisha, "amesema . 

Amebainisha kuwa katika hizo  dawa za kulevya za kumeza wakati mwingine ukishameza lazima uonje kidogo ili uweze kumudu kubeba zile dawa muda mrefu ambapo mwisho wake yule mtoto ambaye anatumika katika kubeba dawa za kulevya na yeye anakuja kuwa mtumiaji wa dawa za kulevya anakuja kuwa mraibu wa dawa za kulevya kwahiyo tatizo la dawa za kulevya linaendelea kuongezeka.


Amesema kuwa  wameshiriki wiki ya sheria nchini wakiwa na  lengo  la kuhakikisha kwamba wanatoa elimu kwa wananchi waweze kuelewa sheria yao namba 5. ya mwaka 2015 kuhusiana na dawa za kulevya  kwamba ukikamwata unajihusisha na dawa za kulevya unazalisha,unasafirisha,unauza,unatumia sheria yao inaweza ikakufunga hadi kifungo cha maisha gerezani hivyo ndiyo maana wapo katika wiki ya sheria kwasababu mahakama ni mdau wao mkubwa katika mnyororo mzima wa haki jinai.

Amesema wanashirikiana na mahakama na taasisi zote za haki jinai katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya sheria yetu ili waweze kujiepusha na biashara ya dawa za kulevya.


Naye Mkaguzi msaidizi wa polisi Verediana Mlimba ni mmoja ya washiriki kutoka jeshi la polisi Tanzania alisema kuwa  wameshiriki katika wiki ya maadhimisho ya wiki ya sheria Tanzania kutokana na ushirikiano walionao na DCEA.


Mlimba amesema wao kama jeshi la polisi wameweka mikakati mbalimbali ambayo kwakiwango kikubwa inawasaidia kuwafikia jamii kwa ujumla mkakati wa kwanza ambao wanashirikiana na DCEA ni Mradi wa usalama wetu kwanza ambao unalenga zaidi watoto ambao wapo mashuleni,kuanzia shule ya masingi sekondari na Vyuo .

"Kwahiyo tulianza kwanza kukemea tulitengeneza kwanza pembe tatu kati ya polisi,mwalimu na mzazi ili kuthibiti utoro halafu tunawapa elimu wao kukataa kuwa wasambazaji kwa nanma yoyote ile kwamaana abebe mzigo kama mtu anampatia ajue amebeba nini na asipojua leo amebeba nini kupeleka wapi basi atoe taarifa kwa mwalimu rafiki ambao ni programu za shule za msingi ama sekondari atoe taarifa leo nilibeba kitu fulani kupeleka sehemu fulani na sikijui ili tuweze kufanya ufuatiliaji alibeba nini na zaidi tunawambia hata kwakutokujua hakikisha unatoa taarifa zote,"amesema.


Hata hivyo amesema wanashirikiana pia na DCEA katika kutambua biashara na kazi zinazofanyika katika maeneo ya shule kwasababu shule zimezungukwa na wajasiriamali wengi hasa zile ambazo hazina uzio .


"Kwa hiyo unakuta kuna mwingiliano mkubwa kati ya watoto na raia kwahiyo tuchokifanya nikuhakikisha tunawatambua wajasiriamali wote ambao wako ndani ya maeneo ya shule tunafanya nao vikao na tumetoa ombi kwa wakuu wote wa shule kuwaomba kwamba wawatambue kwa vitambulisho ili kuepuka muingiliano na  wengine wanaojitokeza, ".

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI