Wanawake wa UWT Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wameadhimisha miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM kwa kupanda miti ya vivuli na miti ya Matunda 107 na kufanya usafi katika Shule ya Sekondari ya Ridhiwani Kikwete iliyopo katika Kata ya Kiwangwa ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM katika mkakati wa kutunza mazingira ya shule hiyo.
Akizungumza wakati wa upandaji miti huo Mwenyekiti wa UWT Mariamu Mkali amesema maadhimisho ya Miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM shughuli mbalimbali za sherehe hizo zinafanyika kwenye Kata hivyo UWT Wilaya ya Bagamoyo wamechagua kupanda miti katika Shule mpya ya Ridhiwani Kikwete.
Mariamu amesema upandaji miti huo umefanywa na Madiwani Viti maalumu, viongozi na Wanachama wa UWT kwa kushirikiana na Wanafunzi wa Shule hiyo.
Hatahivyo UWT walipata nafasi ya kuzungumza na Wanafunzi wa Shule hiyo ya Ridhiwani Kikwete na kukata Wanafunzi wa Shule hiyo kusoma kwa bidii ikiwa ni kuthamini mchango mkubwa wa Wazazi wao kuwasomesha.
Aidha amewataka Wanafunzi hao kumtanguliza Mungu katika masomo yao ili awalinde na vikwazo na changamoto mbalimbali za kukwamisha jitihada zao za masomo ili wafikie malengo yao ya maisha.
Katibu wa UWT Wilaya ya Bagamoyo Catherine Makungwa amesema shughuli zilizofanywa na Wanawake hao wa UWT ni kufyeka nyasi katika maeneo ya shule hiyo, kupanda miti, kuzungumza na Wanafunzi wa Shule hiyo na kutembelea kukagua Maendeleo ya zahanati ya Kata ya Kiwangwa na kushiriki ujenzi wa Moja ya madarasa ya shule hiyo, sambamba na mkutano wa ndani kwa UWT na mkutano wa hadhara uliohusisha wanaCCM na Wananchi kwa ujumla.
++++++++++










0 Comments