Header Ads Widget

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI PROFESA PATRICK NDAKIDEMI AHUDHURIA IBADA KATIKA KITUO CHA SALA CHA MTAKATIFU FRANSIS WA AZIZI, KATA YA OLD MOSHI MAGHARIBI, KIJIJI CHA MANDAKA MNONO



NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ameungana na Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mbokomu katika Kituo Cha Sala cha Mtakatifu Fransis wa Azizi, Kata ya Oldmoshi Magharibi,  Kijiji cha Mandaka Mnono kusali Misa Takatifu ya kuumaliza mwaka wa 2023. 



Mbunge aliandamana na mwenyekiti wa Kijiji cha Mandaka Mnono, Emmanuel Temba.


Baada ya Misa hiyo iliyoongozwa na Paroko Festo Urasa, alipopewa fursa ya kusalimia,  Mbunge Ndakidemi aliwatakia waumini hao heri ya sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya. 



Mbunge aliwapongeza waumini wa Kanisa hilo kwa jitihada zao katika ujenzi wa Kanisa la Mungu na kwa kuguswa na kazi ya ujenzi inayoendelea, Mbunge alitoa mchango wake ili kuunga juhudi za ujenzi wa kanisa hilo.


Padri Urassa alimshukuru Mbunge kwa mchango wake wa kusaidia ujenzi wa Kanisa.



Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI