TAASISI ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Pwani imetakiwa kuendelea kutoa elimu juu ya maadili kwa wananchi na viongozi ili kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini.
Hayo yamesemwa na Hakimu Mkazi mstaafu Mkoa wa Pwani Stephen Mbungu wakati wa tafrija ya kuwapongeza wadau mbalimbali wanaoshirikiana na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwenye mkoa wa Pwani.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dk Abdulsalaam Omar amesema kuwa wanashirikiana na taasisi na mashirika katika utoaji huduma ikiwa ni sehemu ya kuleta maendeleo.
Mwakilishi wa kamishna wa uhifadhi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Mathew Ntilicha amewataka wananchi kulinda mazingira kwa kupanda miti na ufugaji wa nyuki.
Meneja wa Shirika la Ugavi la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Pwani Mhandisi Mahawa Mkaka amesema kuwa wataendelea kushirikiana na taasisi hiyo ili iendelee kuihudumia jamii.
Mwenyekiti wa (CCM) Mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao amesema kuwa elimu inapaswa kutolewa kwa viongozi wakiwemo madiwani na viongozi wa umma kwani baadhi hawana maadili mazuri.
Mhamasishaji wa taasisi hiyo kitaifa Jirabi amesema kuwa lengo kuu ni kuwaunganisha Watanzania ili kujua falsafa za Nyerere ambaye alikuwa akipambana na adui watatu wa Taifa ambao ni Ujinga, Maradhi na Umaskini.
Kwa upande wake katibu wa taasisi hiyo Mkoani Pwani Omary Punzi amesema kuwa wamefanya hafla hiyo ikiwa ni sehemu ya kutoa shukrani kwa wadau mbalimbali ambao imeshirikiana nayo katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
0 Comments