Header Ads Widget

AWESO AIWEKA BODI YA LUWASA LINDI CHINI YA UANGALIZI.

Na Hadija Omary 

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ameiweka katika uangalizi wa mwezi mmoja Bodi ya  Mamlaka ya Maji mjini Lindi (LUWASA) kutokana na kutotekeleza majukumu yake ipasavyo yakufuatilia na kusimamia utendaji kazi wa mamlaka hiyo.


Ametoa kauli hiyo leo januari 26,2024 wakati anazungumza na bodi ,watumishi wa mamlaka hiyo pamoja watumishi kutoka wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini Ruwasa Mkoa wa Lindi.

Hata hivyo Waziri Aweso ameahidi kuleta timu itakayowasaidia huku akiweka bayana maamuzi atakayoyaamua ya kuivunja bodi hiyo endapo haitofanya kazi yake ya kuisaidia mamlaka kwa kuwasimamia watumishi  kufanya kazi kwa weledi na kuboresha huduma .

Aweso pia aliisisitiza bodi hiyo kutimiza majukumu yake ikiwemo  kufuatilia utendaji kazi wa watumishi wa mamlaka jambo litakosaidia kuboreshahali ya upatikanaji wa huduma na kufanya kazi vizuri kama mamlaka zingine za maji  kutoa huduma bora kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI