HADIJA OMARY, LINDI.
ZIKIWA zimepita wiki mbili toka Waziri mkuu Kassim Majaliwa kumuagiza Waziri wa Maji Jumaa Aweso kufika katika ofisi za Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Lindi (RUWASA) na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Lindi (LUWASA) Kufuatilia mapungufu yaliyopo katika ofisi hizo ikiwa pamoja na kutotumika kwa Gari ya uchimbaji wa visima pamoja kutogawiwa kwa pikipiki 22 zilizonunuliwa tangu mwaka 2021 kwa ajili ya jumuiya za watumia Maji za Mkoa huo , Waziri Aweso amefika Mkoani Lindi na kuzigawa pikipiki hizo kwa jumuiya hizo
Tukio hilo limefanyika jana Januari 25 2024 katika ofisi za LUWASA Manispaa ya Lindi huko mkoani Lindi ambapo Waziri wa Maji juma Aweso amewataka wanajumuiya za watumia maji kwenda kutumia Pikipiki hizo kwa malengo yaliyokusudiwa
Mhandisi Muhibu Lubasa ni Meneja wa RUWASA Mkoa wa Lindi amesema Mkoa huo wa una jumla ya skim za maji 340 na jumuiya za watumia maji 82 hivyo kuwepò kwa pikipiki hizo kutaenda kuwarahisishia jumuiya hizo kufanya usimamizi wa karibu katika miradi hiyo ya maji
Nao baadhi ya viongozi wa jumuiya hizo wakaeleza namna pikipiki hizo zitakavyowasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao.
0 Comments