NA CHAUSIKU SAID, MATUKIO DAIMAAPP MWANZA
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya ugawaji wa zana za uvuvi Kwa wavuvi wa Kanda ya ziwa na vikundi mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla ameeleza kuwa rais Samia anatarajiwa kuwasili Mkoa hapa Januari 29 mwaka huu ili kuweza kukabidhi zana hizo za uvuvi.
"Natumia fursa hii kuwakaribisha wananchi wote wa Jiji la Mwanza kujitokeza Kwa wingi katika viwanja ya ndege Kwa ajili ya kumkaribisha rais Samia" Amesema Makalla.
Aidha Makalla amewataka wananchi kujitokeza katika viwanja ya Nyamagana Kwa ajili ya kushuhudia zoezi la ugawaji wa zana hizo Kwa wavuvi wa Kanda ya ziwa.
0 Comments