Header Ads Widget

ALIYEMTEKA MTOTO NA KUDAI MIL 1.5 ATIWA MBARONI

 

Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Almachius Mchunguzi

Na Mbaruku Yusuph Matukio Daima APP, Tanga.

JESHI la Polisi Mkoani Tanga limefanikiwa kumuokoa mtoto mwenye umri wa miaka 3 na miezi 8 aliyetekwa na mtu asiyejulikana na kudai Shs Mil 1.5 ili aweze kumuachia huru.


Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Almachius Mchunguzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio hilo ambalo lilileta sintofahamu kwa wananchi wa maeneo hayo


Kamanda Mchunguzi alisema Jan 23 majira ya saa kumi Jioni Jeshi hilo kupitia vyanzo vyake lilipokea taarifa ya tukio hilo la kutekwa kwa mtoto huyo katika Mji Mpya Wilayani Korogwe ambapo mtoto huyo alipatwa na janga hilo wakati akitokea kucheza katika nyumba ya jirani.

Aidha alisema kufuatia jitihada za Jeshi la Polisi Jan 25 majira ya mchana katika kitongoji cha Sagama 'A' kijiji cha kwamkono, Tarafa ya Sindeo Wilayani Handeni Jeshi hilo lilifanya msako na kufanikiwa kumtia mbaroni Ramadhani Adinai @ Mbano umri miaka 21 mkazi wa Manundu Korogwe akiwa na mtoto huyo.


Kamanda huyo alisema taratibu nyingine za kisheria zinakamilishwa ili mtuhumiwa huyo aweze kufikishwa Mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake huku mtoto akipelekwa kwa wataalamu wa afya kwa uchunguzi na taratibu za kumrejesha kwa mama yake zikifanyika


Kamanda Mchunguzi ametoa wito kwa wazazi/walezi wawalinde watoto wao kwa karibu ili kuwaepusha na vitendo vya watu wenye nia ovu kama vile utekaji,ubakaji na ulawiti kutokupata nafasi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI