Askofu Mteule wa Jimbo Katoliki la Njombe Eusebio Kyando amewasili jioni ya Leo katika Jimbo kuu Njombe
Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Waumini wa Roman Jimbo Katoliki la Njombe Wamejitokeza Kwa Wingi Kumpokea Askofu Mteule Wa Jimbo Hilo Eusebio Kyando Ambaye Aliteuliwa Na Baba Mtakatifu Fracis Kuongoza Jimbo Hilo Akichukua Nafasi Ya Mtangulizi Wake Hayati Askofu Alfred Maluma Aliyefariki Miaka Miwili Iliyopita Kwa Ajali ya gari.
Askofu Kyando Amepokelewa Katika Parokia Ya Kifanya Akitokea Jimbo kuu La Songea Na Baadaye Kulakiwa Tena Na Wananjombe Katika Eneo La Parokia Ya Nundu Mpaka Alipo Wasili Katika Viwanja Vya Kanisa La Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Jimbo La Njombe.
Mamia kwa maelfu ya waumini wameonesha furaha yao kumpata Askofu mpya baada ya kumkosa kwa miaka miwili.
Katika masifu ya jioni ya Leo Askofu huyo mteule amepata fursa ya kuwaahidi Waamini wakatholiki utume uliotukuka mara baada ya kuwekwa wakfu hapo kesho.
Januari 14 siku ya Juma pili hapo kesho Askofu Huyu mteule anawekwa wakfu katika viwanja vya shule ya mtakatifu Bakita na kuanza kuhudumu akiwa Askofu wa tatu wa jimbo Katholiki la Njombe.
Papa Mtakatifu aliyemteuwa Askofu Kyando Amewakilishwa na Balozi wake wa Nchini Tanzania Angelo Accatino.
0 Comments