Watu watatu wamefariki Dunia kufuatia ajali ya Gari iliyohusisha gari aina ya toyota hillux double cabini yenye namba za usajili Sm 14438 kugongana na gari namba T 265 DWP Faw lenye trela no t654 mali ya kampuni ya Felix katika Eneo la kijiji cha mkwajuni kata ya kitomanga barabara kuu ya kitomanga Lindi .
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Lindi John Makuri kwa waandishi wa habari amesema ajali hiyo imetokea jana tarehe January 19/2024 majira ya saa mbili usiku ambapo gari ya Toyota hilux ilikuwa ikitokea Lindi kuelekea kiranjeranje .
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa gari ya Toyota hilux kuhama upande wake wa uendeshaji kushoto na kuhamia kulia ndipo alikutana na lori faw likaja upande wa kulia na kugongana.
Aliwataja watu waliofaliki kuwa ni Ally mwalimba (30) Dereva wa gari toyota hillux mkazi wa Kilwa Masoko, Tumaini Mbando (33) Mtumishi ofisi ya kamishina wa Aridhi mkoa wa Lindi na Farida Mualaga (20) mkazi wa Masasi
0 Comments