Serikali imeamua kuboresha uwanja wa Ndege wa Mwanza kuwa wa kimataifa Kwa kuanza ujenzi na upanuzi wa jengo la kisasa la abiria litakalogharimu sh Bil 30.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla alipotembelea kiwanda cha Samaki cha Nile Perch Fisheries Limited kilichopo Nyakato Jijini Mwanza na kubainisha kuwa baada ya upanuzi wa jengo hilo mizigo yote itasafirishwa moja kwa moja kupitia uwanja huo kwenda ughaibuni.
Makalla amefafanua kuwa pamoja serikali kuleta ndege ya mizigo imeamua kufanya upanuzi wa njia ya kupaa na kutua Kwa ndege ambapo itawasaidia wafanyabiashara kufanya biashara zao Kwa urahisi.
Kwa upande mwingine amebainisha kuwa katika juhudi za serikali kuboresha sekta ya uvuvi, hivi sasa wanahamasisha uvuvi wa kisasa kwa kutumia vizimba na kukomesha uvuvi haramu ili kukuza soko na viwanda vilivyopo mkoani humo.
"TANESCO niwasihi tuboreshe utoaji wa huduma zetu, uzalishaji ukipungua mapato ya nchi yatashuka, ajira kwa watanzania na mitaji pia utapungua hivyo ni lazima muangalie namna ya kuwafanya wenye viwanda wasikwame kwenye uzalishaji." Alisema Makalla.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho Ndugu Rupesh Mohan ameeleza kuwa wamekuwa kiuzalishaji, hivyo wanazalisha tani 15 na wamejipangia kufikisha tani 80.
Mohan ameeleza kuwa wanatumia milioni 200 kulipa ushuru wa huduma, ushuru wa kampuni milioni 150 pammoja na kuchangia zaidi ya Milioni 200 kwenye mifuko ya kijamii kama NSSF, WCF kupitia wafanyakazi 440 pamoja na kodi zingine.
0 Comments