NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR
ZAIDI ya Vijana wanawake elfu 10 wanatarajiwa kupatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masuala ya biashara zenye tija pamoja na kukuza ujuzi na uelewa wa namna bora ya kuinua biashara zao ili lengo la kujiajiri wenyewe bila ya kutegemea ajira kutoka serikalini kufikiwa.
Meneja mradi wa shirika hilo, Lawrence Ambokile, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kuwapatia mafunzo vijana hao ikiwa ni muendelezo wa mafunzo, kwa vijana yaliyoandaliwa na Shirika la Youth challenge International kupitia mradi unaojulikana ‘Her Start’.
Alisema, mafunzo hayo yalianza mwaka 2020 yakiwa yanaendelea hadi sasa yakiwa yanaendelea ikiwemo kuwapatia fedha kuwapatia fedha ambapo mchakato huo unaendelea.
Alisema, pia mradi umelenga kusukuma maendeleo endelevu ya uchumi na kijamii kwa wanawake na jamii zao nchini sambamba na kuondokana na utegemezi na kuweza kujiajiri.
Aidha alisema mradi huo unaendelea kufanya kazi katika nchi tatu ikiwemo Gana, Uganda na Tanzania katika visiwa vya Zanzibar.
Aidha alisema kupitia mradi huo wataweza kuwainua vijana kiuchumi ikiwemo kuwapatia mafunzo ya kubuni jinsi ya kufanya biashara na jinsi ya kuanzisha biashara pamoja na kuwapatia ruzuku kwa lengo la kuanzisha hizo biashara zao walizozilenga.
Hivyo, aliwataka vijana hao kuchangamkia fursa hiyo ambapo taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na serikali ili kuona vijana wanapatiwa mafunzo.
Alifahamisha kuwa kila mwaka wa mradi wanakuwa na malengo husika ikiwemo kuwafundisha vijana ikiwemo kujitambua, kubuni mawazo ya biashara sambamba na kuwasaidia kutengeneza mpango wa biashara.
Nae, Mjumbe anayesimamia Jop la majaji ya uwasilishaji wa mipango ya biashara kwa wajasiriamali wanawake ambao wamepata mafunzo kupitia taasisi hiyo, Mustafa Sharifu, alisema, shughuli hizo zimekuwa na umuhimu sambamba na kusema watahakikisha wanaendeleza vijana katika Nyanja ya ujasiriamali kwani kumekuwepo changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana wengi waliomaliza masomo yao na waliokuwa hawakupata fursa ya kuendelea na masomo ya juu.
Aidha alisema mioongoni mwa changamoto zinazowakumba vijana ni kuweza kutotengeneza mawazo yao ya bishara yakasimama mafunzo hayo yamewasaidia katika kutengeneza mawazo yao kusimama.
‘tatizo kubwa kwa wajasiamali wetu ni kukosa fedha za kuanzisha au mitaji na kuendeleza bisjara zao kwa wale walioshiki miongoni mwao watapata fedha ili kkuweza kuendeleza shughuli zao’ alisema.
Hivyo, alisema matarajio ni kuendelea vijana ili waendeleze biashara hizo sambamba na kutatua changamoto zilizokuwepo katika jamii ambao wajasiliamali wamekuwa wakikosa mitaji kwa ajili ya kuendeleza biashara zao.
Nao, vijana hao, wamesema kupatiwa mafunzo hayo itawawezesha kubuni miradi mbalimbali ili kuweza kuwasaidia sambamba na kulipongeza shirika hilo kwa ubunifu wao sambamba na kuwapatia fedha ili kuendeleza miradi waliyoyaanzisha.
Jumla ya vijana 30 wamehitimu mafunzo hayo na kukabidhiwa vyeti vya kuhitimu sambamba na vijana 10 waliopatiwa awali na kupatiwa fedha ili kuendelea kuimarisha biashara zao walizozianzisha
0 Comments