Mrajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa Kigoma Robert Kitambo akizungumza na viongozi wa vyama vya ushirika kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo wa matumizi ya TEHAMA
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
vyama vya ushirika mkoani Kigoma vimetakiwa kuzingatia jukumu kubwa la kuisaidia serikali kuchochea kasi ya maendeleo, kutengeneza ajira lakini pia kusaidia katika kupunguza umasikini nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa mji wa Kasulu, Julius Buberwa alisema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kujenga uelewa kwa viongozi na watendaji 70 wa vyama vya ushirika mkoa Kigoma kuhusu matumizi ya mfumo wa Habari na mawasiliano (TEHAMA) kwa mfumo wa vyama vya ushirika (MUVU).
Buberwa alisema kuwa Hata hivyo viongozi wa vyama vingi vya ushirika mkoani Kigoma wana utendaji usioridhisha hivyo kushindwa kutekeleza majukumu makubwa ambayo wanayo.
Sambamba na hilo alisema kuwa vyama vingi vya ushirika mkoani humo havina mfumo mzuri wa uandishi wa taarifa za fedha na taarifa za kazi lakini pia vikikabiliwa na kutokuwepo kwa uwazi na uwajibikaji hivyo mafunzo hayo yanaweza kujibu changamoto hizo.
Awali akitoa maelezo kwenye ufunguzi huo, Mrajiisi Msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa Kigoma, Robert Kitambo alisema kuwa zaidi ya makatibu na mameneja wa vyama vya ushirika 70 kutoka halmashauri nane za mkoa Kigoma wanahudhuria mafunzo hayo.
Kitambo alisema mafunzo ya siku tatu yanayolenga kuwajengea uwezo wa kuandika na kutuma taarifa za fedha na taarifa za kazi kutumia mfumo wa teknolojia ya dijitali wa ushirika unaojulikana kama MUVU kuondona na kuzunguka na mafaili kupeleka taarifa zao kwenye mamlaka mbalimbali za serikali.
0 Comments