NA HAMIDA RAMADHANI, MATUKIO DAIMA AAP DODOMA
KAIMU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Anamringi Macha amewataka Wajumbe wa Jumuiya ya wazazi kutunza siri za vikao vya Chama lengo likiwa ni kuendelea kukilinda Chama na taifa Kwa ujumla.
Macha ameyasema hayo leo Desemba 6, 2023 Jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Baraza kuu la Jumuiya ya wazazi Chama cha Pinduzi CCM.
Amesema katika vitu ambavyo vinaweza kuharibu mustakabari wa Chama ni pamoja na wajumbe kutokuwa na Siri ya yale yote yanayoelekezwa na kukubaliana nadani ya vikao vya chama.
" Niwaombe tutunze Siri za vikao vyetu vya chama pindi tunapokutana na kufanya vikao vyetu ili kukilinda chama Chetu Cha Mapinduzi na Taifa la Tanazania kwa ujumla,"amesema Macha
Aidha akizungumzia suala la maadili amesema ili kukemea maadili mabovu kwa vijana ni wazi sasa kama wazazi kutafakari mienendo yao kama inafaa ili kuweza kuwasaidia vijana na jamii Kwa ujumla.
Hata hivyo amewataka baadhi ya watu wanaotumika kuivuruga jumuiya hiyo kuacha mara moja jambo hilo kwa kuwa ni la aibu .
"Badala yake fanyeni kazi Kwa kufuata kanuni , Taratibu huku mkivumiliana, kupendana na Kwa ushirikiano ili kuijenga imara jumuiya na Chama kwa ujumla," amesema .
Amesema ili jumuiya hiyo irudi katika ubora wake ni wakati sasa wakuongeza juhudi, nakufanyakazi kwa kupendana , Kuvumiliana na kwa kushirikiana
" Tutumie vikao kujadili mambo yetu, kama Kuna watu wachache wapo kwaajili ya kuivuruga jumuiya hii tusiwape nafasi na tukishindwa kufanyakazi Kwa Kuvumiliana basi tufuate kanuni ," ameeleza Macha.
Na kuongeza kusema" Na sisi kama Chama hatutokubali kuanza kufikiriana fikiriana , tutafute mambo ya msingi kuijenga jumuiya tusianze chokochoko, " amesema Macha.
Naye Makamu Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Dogo Iddi Mabrouk ameendelea kusisitiza juu ya utunzaji wa siri nakuwataka wajumbe hao kuacha mambo ya kitoto nawafanye mambo kama watu wazima.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa jumuiya hiyo Fadhil Maganya amesema jumuiya hiyo imesikitishwa na maafa yaliyotokea katika Kijiji cha Katesh Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara kufuatia vifo na watu wengine kujeruhiwa kutokana na kunyesha Kwa mvua na kusababisha mafuriko ya matope na kusema kama jumuiya desemba 6, 2023 itaungana na viongozi wengine kutoa pole na faraja ikiwemo bidhaa za chakula Kwa wahanga hao.
Kikao hicho Cha Baraza Kuu la Jumuiya ya wazazi ni cha siku moja na kimehudhuriwa na wajumbe 109 kati ya wajumbe halali 145.
0 Comments