Header Ads Widget

VIN DIESEL ASHTAKIWA KWA UNYANYASAJI WA KINGONO DHIDI MSAIDIZI WAKE

 


Nyota wa "Fast & Furious" Vin Diesel anashutumiwa kwa unyanyasaji wa kingono na msaidizi wa zamani.

Katika kesi iliyowasilishwa Los Angeles Alhamisi, Asta Jonasson anadai kuwa mwigizaji huyo alimnyanyasa kijinsia msimu wa 2010 wakati wa kurekodi filamu ya "Fast Five" huko Atlanta.

 

Kwa mujibu wa kesi hiyo, Jonasson aliajiriwa na kampuni ya utayarishaji filamu ya muigizaji huyo ya One Race ili kumfanyia kazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuandaa na kumsindikiza Diesel kwenye tafrija na kuhakikisha yuko karibu kwenye picha ikiwa mwigizaji huyo alihudhuria hafla bila mpenzi wake wa muda mrefu.

 

Wakili kutoka Greenberg Gross, kampuni inayomwakilisha Jonasson, alisema katika taarifa yake: "Tunajivunia kumwakilisha Bi. Jonasson na kumwajibisha Vin Diesel na wale walioruhusu na kuficha unyanyasaji wake wa kijinsia. Sheria ipo kuwalinda wale ambao wamekuwa wakidhulumiwa, haijalishi mshtakiwa ana nguvu au umaarufu kiasi gani. Unyanyasaji wa kijinsia mahali pa kazi hautakoma kamwe ikiwa wanaume wenye nguvu watalindwa dhidi ya uwajibikaji."

 

Bryan Freedman, wakili wa Los Angeles anayemwakilisha Vin Diesel, alisema katika taarifa kwamba Diesel "anakanusha madai hayo yote kwa ukamilifu."

 

"Hii ni mara ya kwanza kwake kusikia kuhusu madai hayo ya zaidi ya miaka 13 yaliyotolewa na mfanyakazi anayedaiwa kuwa wa siku 9," Freedman alisema katika taarifa hiyo. "Kuna ushahidi wa wazi ambao unakanusha kabisa madai haya ya ajabu."

 

Madai hayo yanaeleza kuwa baada ya usiku wa Septemba 2010, Jonasson aliombwa kumsubiri Diesel, 56, katika chumba chake ndani ya hoteli ya St. Regis, Diesel alishika viganja vya Jonasson na kumvuta kitandani, kwa mujibu wa kesi hiyo.

 

Alimuonya na kumtaka Diesel aondoke, lakini inadaiwa alianza kupapasa matiti yake, kumbusu kifuani na kumshika kiunoni na juu ya miguu yake, yakiwemo mapaja ya ndani.

 

Jonasson aliogopa "kumzuia mkuu wake" kwa usalama wake binafsi na usalama wa kazi, lakini baada ya Diesel kusogea kushusha chupi yake, Jonasson alipiga mayowe na kukimbia.

 

Kulingana na kesi hiyo, Diesel alimbana ukutani na kuweka mkono wake kwenye sehemu zake za siri. Alipiga punyeto, huku "akiwa na hofu, Bi. Jonasson alifumba macho, akijaribu kujitenga na unyanyasaji wa kijinsia na kuepuka kumkasirisha," kulingana na kesi hiyo.

 

Saa chache baadaye, dadake Diesel na rais wa One Race Samantha Vincent alimpigia Jonasson kumfukuza kazi baada ya kukaa kazini kwa muda usizidi wiki mbili kazini, shauri hilo linasema.

 

 

Chanzo; USA TODAY

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI