Header Ads Widget

TAKWA LA RAIS SAMIA LAENDELEA KUTEKELEZWA eGA

Na Hamida Ramadhani, Matukio Daima APP Dodoma

MAMLAKA ya Serikali Mtandao (eGA) imeendelea kutekeleza agizo la Rais wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha mifumo ya TEHAMA katika taasisi za umma zinauganishwa na kubadilishana taarifa kidijitali ambapo mpaka sasa Mamlaka imefanikiwa kujenga mifumo mitatu huku jumla ya taasisi za umma 109 zimeuganishwa katika mfumo wa GovESB  na mifumo 117 imeshasajiliwa. 


Mifumo hiyo iliyojengwa ni pamoja na Mfumo Mkuu wa ubadilishaji taarifa Serikali ( GovESB), Mfumo wa pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji wa Shehena maeneo ya forodha( Tanzania Electronic Single Window System -  TeSWS) na Ubadilishaji wa Taarifa katika Mifumo ya TEHAMA ya Serikali na sekta Binafsi. 

Akiongea leo jijini Dodoma kwenye mkutano na waandishi wa Habari juu ya Utekekezaji wa Jitihada za mifumo ya TEHAMA ya Taasisi za umma kubadilishana taarifa kidigital Mhandisi Benedict Ndomba Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Serikali Mtandao eGA amesema Mfumo wa GovESB umetengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao eGA kwa kuzingatia sheria inayoitaka eGA kuanzisha na kuendesha Mfumo unaowezesha mifumo ya TEHAMA Serikali kuwasiliana na kubadilishana taarifa kidijitali. 


"Ujenzi wa Mfumo wa (GoVESB) ni Utekelezaji wa agizo la Rais, Dkt, Samia Suluhu Hassan kuhakikisha mifumo ya TEHAMA katika taasisi za umma inauganishwa na kubadilishana taarifa, " Amesema Mhandisi Ndomba. 

Mfumo wa ubadilishanaji wa Taarifa Serikali ni mfumo wa Kielektroniki unaouganisha mifumo ya TEHAMA ya taasisi za umma iweze kusomana na kubadilishana taarifa kila inapohitajika. 


" Lengo la mfumo huu ni kuziwezesha  taasisi za umma kubadilishana taarifa kidijitali kwa usalama, kupunguza urudufu  wa mifumo kuongeza ufanisi wa utendaji kazi, kupunguza gharama za uendeshaji pamoja na kuokoa muda kwa kuwa taarifa hupatikana kwa wakati, " Amesema Mhandisi Ndomba. 


Hata hivyo Mhandisi Ndomba amesema kabla ya kuanza kutumika kwa mfumo wa GovESB kulikuwa na Changamoto za ubadilishanaji wa taarifa katika taasisi za umma zikiwemo kutumia muda mrefu kupata taarifa kwani taasisi zililazimika kuwasilisha maombi ya kupata Taarifa inayohitaji kwa kwa njia ya barua katika taasisi husika. 


" Utaratibu huu wa barua ulichukua muda mrefu kupata Taarifa hizo jambo liliochangia kupunguza ufanisi katika utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wananchi, " Amesema. 


Na kuongeza " Changamoto nyingine ilikuwa utofauti wa utaratibu wa kupata Taarifa kutoka taasisi moja Hadi nyingine kwani kila taasisi inao utaratibu wake wa ndani wa kupata na kutoa taarifa na wakati mwingine utaratibu hubadilika, " Ameeleza Mhandisi Ndomba. 

Katika mfumo wa pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji wa Shehena maeneo ya Forodha ( TeSWS) Mhandisi Ndomba amesema mfumo wa TeSWS ni scheme ya Utekekezaji wa kuboresha Mazingira ya biashara nchini_ MKUMBI (Blueprint) ambapo mfumo utawawezesha wa fan ya biashara kukamilisha maombi ya vibali na maandalizi ya malipo  ya Kodi za forodha

Kidijitali bila kwenda kwenye taasisi za Udhibiti wa forodha na hivyo kuongeza ufanisi na utendaji kazi. 


Katika ubadilishanaji wa taarifa kati ya Mifumo ya TEHAMA ya Serikali na ya sekta Binafsi unawezesha kadiri ya mahitaji yanavyohitajika. 


" Mathalani mfumo wa malipo ya Serikali GePG umeuganishwa na Benki zote nchini pamoja na makampuni yote ya simu za mkononi ili kuwezesha huduma ya malipo ya Serikali kupitia simu za mkononi, " Amesema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI