Header Ads Widget

MWALIMU JELA MIAKA MITATU KWA KUSHAWISHI KUTOA RUSHWA KWA AFISA UTUMISHI



ABDALA AMIRI  MATUKIODAIMA App IGUNGA

Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu Mwalimu Jesca Jones Yegera (60) mkazi wa Mtaa wa Mwanzugi Kata ya Igunga mjini miaka mitatu jela kwa ma kosa mawili ya kushawishi kutoa rushwa ya Sh laki 5 kwa Afisa Utumishi.


 Jesca ambaye ni mwalimu mstaafu wa Shule ya Msingi Mwanzugi alipatikana na hatia baada ya Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Igunga, Mazengo Joseph kuiambia Mahakama  ya Hakimu wa Wilaya Edda Kahindi kuwa  mshitakiwa alitenda makosa hayo mawili Juni, 24 mwaka 2022.


Mwendesha mashitaka alidai kuwa tarehe hiyo majira ya mchana akiwa kwenye ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, mshtakiwa alimshawishi kumpatia rushwa ya Sh. Laki kwa njia ya simu Afisa Utumishi  Mwandamizi Erick Sije (38) anayefanya kazi katika Halmashauri ya wilaya ya Igunga.


Mazengo alidai mshitakiwa huyo alishawishi na kutoa rushwa kiasi cha Sh laki 3 kati ya s

Sh. laki 5 alizoahidi kwa njia ya simu ili aweze kumsaidia kupata madai yake ya malimbikizo ya mishahara ya miezi mitano aliyokuwa anadai toka Serikalini kiasi cha sh. 6,175,000.


Alidai kuwa  mshitakiwa huyo alitenda makosa hayo mawili kinyume na kifungu cha 15 (1) (b) (2) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura 329 mapitio ya 2019 inayozuia kutenda makosa kama hayo.


Hata hivyo baada ya kusomewa mashitaka hayo mawili, mshitakiwa alikana kutenda makosa hayo mawili na ndipo upande wa mashitaka ulipeleka mashahidi sita mahakamani ambao walitoa ushahidi mahakamani.


Ambapo upande wa mshitakiwa alikuwa na mashihidi wawili yeye na mume wake ambao walitoa ushahidi mahakamani.


Hata hivyo baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili Hakimu Edda kahindi aliridhika pasipo shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri na umemuona mshitakiwa Jesca Jones Yegela ana hatia.


Hivyo Mahakama inamhukumu kulipa faini ya sh. 1,000,000 na akishindwa kulipa atakwenda jela miaka mitatu ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia hiyo. Hata hivyo hadi mwandishi wa habari hii anaondoka Mahakamani mshitakiwa alikuwa bado hajalipa faini huku akibaki chini ya ulinzi wa polisi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI