MATUKIODAIMA APP, Lindi
Mkuu wa wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai ameonya tabia ya wazazi kuruhusu watoto kwenda kwenye mabanda ya video.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya kampeni ya siku 16 ya kupinga vitendo vya ukatili katika kijiji cha Namayuni Tarafa ya Kipatimo Wilayani kilwa.
Ngubiagai alisema kuwa watendaji wa vijiji , kata pamoja na vitongoji kuhakikisha kuwa mabanda ya video yanafungwa,kwani ndani ya mabanda hayo yamekuwa yakifanyika michezo ya ajabu .
"Kwenye mabanda haya ya video watoto wakike wanalipiwa hela na vijana wa kiume,halafu wakifika ndani wale vijana wanawapakata wale watoto wa kike na kuonesha mikanda ya video ,isiofaa kwa maadili ya kitanzania."Amesema DC
"Niwaombe Watendaji wa kijiji ,atakaye shindwa kusimamia jambo hili hana nafasi ya kufanya kazi katika wilaya ya yangu na wote watachukuliwa hatua kali za kisheria , hatuwezi kila siku tukawaharibu watoto,kwa uzembe wa watu wachache."Amesema pia
"Hawa watoto kila siku wanaingia kwenye mabanda yavideo wanapata wapi pesa kama sio wanalipiwa kwa nini ulipiwe anaye lipa anakupendea kitu gani hakuna kitu cha bure dunian anaye kulipia kuna kitu ana kitaka akikwambia twende utakataa"amesema Ngubiagai.
Pia amewataka wazazi kuacha tabia ya kuficha taarifa za vitendo vya ukatili ,amesema atakaye gundulika atamchukuliwa hatua kuanzia baba,mama,mtoto na hadi aliefanya kitendo hicho mwenyewe.
Nae mwezeshaji kutoka shirika la Tcrs Mzava Sailasi amesema kuwa kabla ya wao kuanzisha uhamasishaji wa kupinga vitendo vya ukatili ,matukio ya ukatili,utiaji mimba,na ulawiti,yalikuwa nimengi mno ,ila kwa sasa jamii imeshaanza kuwa na uelewa juu ya maswala ya ukatili,na kupungua kwa matukio hayo.
"Tokea tumeanza mradi mwaka 2017 uwelewa wa wananchi umekuwa mkubwa sana hata taarifa za matukio zimepungua japo bado ukatili unaendelea mwanzo tulikuta kama asilimia 80 ila kwa sasa ipo chini ya asilimia 50 kwani kwasasa kwamwezi tunaweza pokea kesi 3 kwa mwezi na tusipokee tena hadi miezi 3 baadae"amesema Mzava.
Amesema pia , walianza kwakuwapa elimu ya kujitambua kuna vijana wamewatengeneza wanashugulikia maswala yote ya ukatili katika jamii,hadi 2025 wanategemea maswala ya ukatili wa kijinsia na yanayofanana na hayo yawe yamekoma kabisa.
Hawa Mbonde ni mkazi wa kata ya Namayuni amesema hali ya ukatili ipo lakini bado wanajificha ficha wanaogopana wenyewe kwa wenye.unakuta aliye fanyiwa ukatili ni mjukuu wangu aliye fanya ni mwanangu natoaje taarifa aje mgeni ndiyo aje asimamie naiyonekane mgeni ndiyo aliyetoa tarifa sio sisi wenyewe.
"Kutoa taarifa kwa uongozi inakuwa ngumu,unakuta mim kizazi changu ndicho kilichofanyiana ukatili,mfano mwanangu amemfanyia ukatili mjukuu wangu,wote ni familia moja naendaje kushtaki,akifungwa mwanangu,hasara si kwangu,sasa inabidi haya mashirika yajitahidi kuja kufichua ukatili ila sio sisi wenyewe,itakuwa ngumu".Amesema Hawa
Kampeni ya siku 16 za kupiga ukatili wa kijinsia Wilayani Kilwa shirika la TCRS kwa kushirikiana na Norwegian Church Aid (NCA) limeto elimu ya ukatili wa kijinsia na kuwataka wanawake kuwalinda watoto wao ili wasipate matatizo ya ikatili,kwa kuwanao karibu wakati wowote ,ilikuweza kuwaepusha na vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikiharibu ndoto za watoto wakike.
0 Comments